Latest Posts

KESI YA WENDY: MADELEKA ALIVYOMBANA INSPEKTA WA POLISI/ UHIFADHI WA USHAHIDI WALETA MASWALI

Agosti 7, 2026 Kesi ya Uhujumu uchumi Na. 4521/2026 inayomkabili Wendy William Ishengoma na wenzake wanne imeendelea Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi, Dar es Salaam ambapo shahidi wa pili wa jamhuri Inspekta Michael Mwakalikamo (40) ameendelea kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji Dkt. Dafina Ndumbaro anayesikiliza kesi hiyo.

Akiongozwa na Mawakili wa Jamhuri Inspekta Michael alimalizia mahojiano ya awali ya ushahidi (examination in chief) kisha baadae upande wa utetezi kupitia Wakili Peter Madeleka na Wakili Grey Godifrey Dedan walipata kumuuliza shahidi maswali ya dodoso(Cross-examination).

Shahidi alidai mahakamani kuwa kampuni ya Atlantic Microcredit Ltd. ambayo ni mshtakiwa wa tano ilikuwa ikifanya ulaghai kwa wateja wao kwa kuwaambia wanawekeza huku wakipewa faida ya 40% ndani ya siku 25 hata hivyo amedai kuwa pindi walopohojiwa washtakiwa kuaw wanawekeza fedha hizo kwenye nini walisema ni kwenye biashara ya kubadilishana fedha(Forex trading) na sarafu mtandao(cryptocurrency) jambo ambalo anasema walishindwa kulithibitisha pindi walipopewa kompyuta na intaneti.

Alipohojiwa na Wakili Madeleka  juu ya kama watu waliowekeza kwenye kampuni hiyo walilalamika kuhusu kulaghaiwa shahidi alisema taarifa walizipata kwa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) hata hivyo wapo waliolalamika lakini hawajui na hakuwaweka kweye ushahidi kwa sababu si sehemu ya ushahidi wake.

Kuhusu utunzaji wa vielelezo shahidi alieleza kuwa vielelezo hivyo alikabidhiwa Mahakamani na Wakili wa Serikali Mkuu Mwahija jambo ambalo Madeleka alisema ataiomba mahakama apate nafasi ya kumdodosa aliyeleta vielelezo mahakamani.

Wakili: Mweleze jaji mara baada ya kukamilisha upelelezi vielelezo ulipeleka waoi

Shahidi: Nilikabidhi kwa inchaji wangu wa upelelezi na baadhi nilikuwa na access navyo, sehemu ya vielelezo vilikuwa vinakaaa jaladani hasamwa documentary evidence.

Wakili: Unakubaliana na mimi kwamba jalada la vielelezo lilikabidhiwa kwa waendesha mashtaka

Shahidi: Katika ushahidi wangu hakuna sehemu nikitaka

Wakili: Leo unajua ulitoa vielelezo kutoka kwa waendesha mashtaka

Shahidi: Sahihi

Wakili: Tutaiomba mahakama itoe amri kwa huyi mwendesha mashtaka kwa huyu alieyeleta vielelezo.

Pamoja na hayo alihojiwa juu ya kurekodi maelezo ya washtakiwa aliowahoji ambapo alikiri kurekodi baadhi ya maelezo na yapo ambayo hakurekodi na mengine alirekodi kwenye notebook yake ambayo aimesahau ilipo.

Wakili: Ni sahihi uliwahoji washtakiwa ulirekodi

Shahidi: Kuna mahojiano ya mdomo na ya kuandika

Wakili: Unataka kusema polisi anaruhusiwa kwa mdomo

Shahidi: Professionally

Wakili: Mahakama inathibitishaje

Shahidi: Kwa ushahidi niliotoa

Wakili: Haya ya Forex hukuona haja ya kuandika

Shahidi: Niliandika kwenye notebook ambayo sikumbuki iko wapi

Aidha juu ya kama kampuni ya kama kampuni hiyo imewahi kushtakiwa kwa kosa lolote alieleza kuwa hapana ndiyo mara ya kwanza huku akikiri kuwa BOT haijawahi kuharamisha shughuli inayofanywa na kampuni hiyo.

Wakili: Kama hawajakubaliana inakuwa ni kosa chini ya kifungu gani

Shahidi: Mheshimiwa jaji sijasema kwamba kukata bima ni kosa nimesemaregulatory authority(malaka ya uthibiti) ambayo ni BOT iinataka taasisi za kifedha kuwa na bima

Wakili: Kuna mahakama imewahi kuthibitisha Atlantic kufanya shughuli za kihalifu

Shahidi: Hapana

Wakili: Ni mara ya kwanza Atlantic inaletwa hapa

Shahidi: Ndio

Wakili: Kwa hiyi si wahalifu

Shahidi: Ndio maana nipo hapa kuthibitisha

Hata hivyo maswali ya dodoso hayakufika mwisho kutokana na muda kuwa hafifu(shauri liliisha saa kumi na mbili jioni kasoro) na shauri hilo liliahirishwa mpaka Agosti 13-14, 2026 ambapo litaendelea tena mahakamani hapo huku vielelezo vingine vikibaki chini ya Mahakama na magari mawili Toyota Alphard yakirudi kuhifadhiwa Ofisi ya Mashtaka.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!