Latest Posts

INEC YATOA ONYO KALI KWA WATAKAO JIANDIKISHA MARA MBILI DAFTARI LA MPIGA KURA

Tume huru ya uchaguzi imewataka wananchi watakaokuwa na sifa ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura kutojiandikisha mara mbili kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai ambalo litawapelekea kufungwa au kupigwa faini kwa mujibu wa sheria .

Katika uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura,kwa chaguzi zilizopita Tume huru ya uchaguzi ilibaini majina ya watu walijiandikisha zaidi ya mara moja 52078 kwa mwaka 2015, na mwaka 2020 Jumla ya wapiga kura 43,301 walijiandikisha ambapo kwa ujumla wao walifikishwa kwenye Vyombo vya Dola na kufinguliwa kesi ya jinai.-

“Yapo maneno ya upotoshaji ambayo baadhi ya vyama vya siasa vimeanza kutoa kwamba,mfumo wa uandikishaji wa tume unaruhusu kuandikisha mpiga kura zaidi ya mara moja,Na kwa kusisitiza hoja yao wameonesha kadi ambayo ni ya Andrew Kitungi mwenye Kadi namba T-1003-3617-715-9 yenye jina la tume ya taifa ya uchaguzi na kadi nyingine yenye namba hiyo hiyo yenye jina la tume huru ya uchaguzi tayari hatua zimeshachuliwa kwa mhusika”alisema Jaji Jacobs Mwambegele.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi ,Jaji Jacobs Mwambegele wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Geita kuelekea kwenye zoezi la uandikishaji linalotarajia kuanza tar 5 August 2024.

“Yapo maneno ya upotoshaji ambayo baadhi ya vyama vya siasa vimeanza kutoa kwamba,mfumo wa uandikishaji wa tume unaruhusu kuandikisha mpiga kura zaidi ya mara moja,Na kwa kusisitiza hoja yao wameonesha kadi ambayo ni ya Andrew Kitungi mwenye Kadi namba T-1003-3617-715-9 yenye jina la tume ya taifa ya uchaguzi na kadi nyingine yenye namba hiyo hiyo yenye jina la tume huru ya uchaguzi tayari hatua zimeshachuliwa kwa mhusika”alisema Jaji Jacobs Mwambegele.

Aidha Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Taifa,amewataka wananchi ambao wanakadi za kupigia kura zilizotolewa kwa Jina la TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI wanaofika vituoni kutaka kupata kadi zenye jina la TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI na kwamba ni vyema wakaendelea nazo za awali kwani hazina tatizo lolote.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!