Latest Posts

MAAFISA WA ZIMAMOTO WA AFRIKA KUSINI WAFARIKI KWA MOTO WAKIZIMA MOTO

Maafisa sita wa kikosi cha zimamoto wamefariki dunia walipokuwa wakipambana na moto katika jimbo la KwaZulu-Natal mashariki mwa Afrika Kusini na wengine wawili wako katika hali mbaya kwa mujibu wa taarifa ya Jumatatu ya idara ya huduma za dharura.

Kulingana na kituo cha habari cha VOA, mamlaka zinashuku kuwa moto huo wa siku ya Jumapili huenda uliwashwa na wawindaji haramu wanaojaribu kuwanasa wanyama na kuwaua.

Msemaji wa huduma za dharura Roland Robertson amesema maafisa watatu wa kikosi cha zimamoto wamefariki dunia katika eneo la moto karibu na mji wa Boston uliopo kilomita 130 kutoka pwani ya mashariki ya jiji la Durban.

Ameongeza kuwa maafisa wengine watatu walitibiwa na kuwekewa mashine za kupumulia, lakini wote walifariki dunia mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo na kwamba afisa mmoja bado yuko kwenye mashine ya kupumulia hospitalini, na mwingine pia yuko katika hali mbaya.

Robertson amesema baadhi ya majangili pia wanasadikiwa kujeruhiwa katika moto huo karibu na mashamba ya watu binafsi kutokana na upepo na ardhi kavu kuwafanya kuteketea bila kudhibitiwa huku kukiwa hakuna ripoti za kukamatwa kwa washukiwa wa ujangili.

Moto wa msituni umewaka katika maeneo mengine ya KwaZulu-Natal wiki iliyopita kutokana na joto na upepo, ambao umesababisha vifo vya watu wengine saba katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, serikali ya eneo hilo imesema.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!