Latest Posts

SANGU AHAMASISHA WADAU KUWEKEZA KWENYE ELIMU

Wadau wa maendeleo ndani na nje ya Mkoa wa Rukwa wamehamasishwa kuchangia upatikanaji wa madawati ili kuwezesha watoto kusoma katika mazingira bora na rafiki ya kujifunzia, yatakayochangia kuboresha ustawi wa taaluma.

‎Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mbunge wa Jimbo la Kwela, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Kazini, Deus Sangu, alipokabidhi madawati kwa shule za msingi za jimbo hilo katika ziara yake ya kikazi.

‎

‎Akizungumza katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Kijiji cha Nankanga, Tarafa ya Kipeta, na Kijiji cha Ilemba, Sangu amesema msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za wananchi katika kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu, huku akisisitiza kuwa mazingira bora ya kujifunzia ni msingi muhimu wa kuinua kiwango cha elimu kwa watoto.

‎Katika ziara hiyo,  Sangu amekabidhi zaidi ya madawati 100 kwa shule sita (6) za msingi, yenye thamani ya shilingi milioni 60. Madawati hayo yamepatikana kupitia ufadhili wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!