Latest Posts

WATU WATATU WAFARIKI KWA KUJINYONGA WILAYANI MOSHI, CHANZO CHATAJWA

Watu watatu wa jinsi ya kiume wamefariki dunia kwa kujinyonga katika matukio tofauti yaliyotokea wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro, akiwamo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kotela Mashariki, Lamecky Matowo (57).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa matukio hayo leo tarehe 23 Julai 2026, akibainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonesha matukio hayo yameshochewa na changamoto za afya ya akili na msongo wa mawazo.

Kamanda Maigwa ameeleza kuwa Mwenyekiti Matowo alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila aliyofunga kwenye mti uliopo shambani kwake.

Mbali na kiongozi huyo, wengine waliofariki ni Frank Makundi (54); fundi ujenzi na mkazi wa Kijiji cha Komakundi, Kata ya Mamba Kaskazini, na Januari Hussein (30); dereva wa pikipiki za abiria (bodaboda) na mkazi wa Kimaroroni.

Akifafanua kuhusu nyakati na visababishi vya vifo hivyo, Kamanda Maigwa amesema matukio mawili yalitokea tarehe 22 Julai na jingine lilitokea tarehe 21 Julai 2026 na kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa Matowo alichukua uamuzi huo kutokana na changamoto ya afya ya akili. Kwa upande wa Makundi, naye alijinyonga kutokana na msongo mkubwa wa mawazo uliotokana na msiba wa mtoto wake aliyefariki miezi miwili iliyopita.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi bado unaendelea kubaini chanzo kamili cha kifo cha Januari Hussein, huku likitoa rai kwa jamii kutafuta msaada wa kisaikolojia wanapokabiliwa na changamoto za afya ya akili badala ya kuchukua maamuzi yanayogharimu maisha yao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!