Latest Posts

MBUNGE KISWAGA ATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA TOSAMAGANGA

Na Mwandishi Wetu – Kalenga, Iringa

Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Mheshimiwa Jackson Kiswaga, ameendeleza moyo wa huruma kwa jamii kwa kutembelea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Tosamaganga, ambapo ametoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya malezi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho.

Ziara hiyo ambayo ni ya pili kwa Mbunge Kiswaga katika kituo hicho, imelenga kuunga mkono jitihada za kuwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, sambamba na kuhamasisha jamii kushiriki katika kuwasaidia watoto hao.

“Ninawaomba wananchi wote waendelee kuwa na moyo wa huruma na upendo kwa watoto hawa. Tuwaone kama sehemu ya familia zetu. Kuwasaidia ni wajibu wetu kama jamii yenye utu,” alisema Mbunge Kiswaga wakati wa kukabidhi msaada huo.

Msaada uliotolewa ni pamoja na vyakula, mavazi, vifaa vya usafi na mahitaji mengine muhimu kwa ustawi wa watoto hao.

Kwa upande wake, msimamizi wa kituo hicho, Sista Hellena Kihwele, alisema kituo hicho kwa sasa kinahudumia jumla ya watoto 150, ambapo watoto 85 ni wakazi wa kudumu katika kituo hicho. Sista Hellena alimshukuru Mbunge Kiswaga kwa moyo wake wa kujitoa kusaidia jamii, hususan watoto wanaohitaji uangalizi maalum.

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kuwa pamoja nasi tena, msaada wake ni wa thamani kubwa kwenye malezi ya watoto hawa,” alisema Sista Hellena.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!