Latest Posts

MJUMITA WATAKIWA KUSAMBAZA ELIMU YA UHIFADHI WA MISITU YA ASILI KWA WATOTO

Wanajumuiya ya Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) wametakiwa kusambaza elimu ya uhifadhi wa misitu ya asili waliyonayo kwa watoto wadogo ambao ndio kizazi tegemewa kwa uhifadhi endelevu wa misitu.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula alipokuwa akifungua warsha na mkutano wa mwaka wa jumuiya hiyo katika ukumbi wa Edema Manispaa ya Morogoro.

Kitandula ameongeza kuwa Tanzania inapoteza zaidi hekta ya 469,000 za misitu kwa mwaka, hivyo zinatakiwa juhudi za makusudi ili kuweza kunusuru misitu ya nchi.

“Ninapenda kutoa wito kwa wote, kila mmoja wetu achukue nafasi yake katika kuitetea misitu yetu, ni lazima tukumbuke kuwa uhifadhi si kazi ya mtu mmoja au kikundi kimoja, ni jukumu la kila mmoja wetu, kuanzia kwenye ngazi ya familia zetu hadi kwa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kwani kwa pamoja, tunaweza kulinda misitu yetu”, ameeleza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!