Latest Posts

MTOTO ALIYEPEWA RUFAA KUTOKA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA AANZA MATIBABU MOI

Taasisi ya tiba ya mifupa na ubongo Muhimbili (MOI) imeanza kutoa matibabu ya kibingwa kwa mtoto Godson Mwaipopo (7) ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa kambi ya matibabu ya kibingwa yaliyokuwa yanafanyika mkoani Arusha

Mtoto Godson ni miongoni mwa maelfu ya watoto na watu wazima waliogundulika kwenye kambi hiyo ya matibabu iliyokuwa ikiratibiwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amejitolea kugharamia matibabu ya wagonjwa wote waliopatiwa rufaa kupelekwa kwenye Hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili

Joyce Mwasakapwela ni mama mzazi wa mtoto huyo ambaye amesafiri na mwanaye kwenda MOI, jijini Dar es Salaam kusimamia matibabu ya mwanaye akiambatana na mume wake Isaac Mwasakapwela kwa gharama za Mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo katika maeneo yake ya shukrani ameelekeza kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa mkoa wa Arusha na wananchi waliomchangia nauli ya kutoka mkoani Mbeya awali ili kuifuata kambi ya matibabu mkoani Arusha ambapo amsema anaamini kuwa mtoto wake atarejea katika hali yake ya kawaida.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!