Latest Posts

SERIKALI YACHUKUA HATUA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO VINAVYOZUILIKA

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Florence Samizi, amesema serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto, kwa lengo la kupunguza na hatimaye kukomesha vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama wajawazito na watoto wachanga nchini.

‎Dk.  Samizi ameyasema hayo leo, Agosti 11, 2026, wakati akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Afya mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI kuhusu hali ya vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga pamoja na mikakati ya Serikali ya kukabiliana na changamoto hiyo.

‎Amesema hatua hizo zinahusisha kuimarisha miundombinu ya huduma za afya ya uzazi na watoto wachanga, kuongeza vituo vyenye uwezo wa kutoa huduma za dharura za uzazi na mtoto, pamoja na kuboresha Wodi Maalum za Watoto Wachanga (NCU) katika hospitali mbalimbali nchini nakuongeza kuwa serikali imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba muhimu, oksijeni na huduma nyingine za kuokoa maisha, hususan kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati au wenye changamoto za kupumua.

‎Dk.  Samizi amesema serikali pia imeongeza wataalamu wenye ujuzi katika huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto, huku ikiendelea kuwajengea uwezo watoa huduma ili waweze kutambua mapema viashiria vya hatari na kuchukua hatua kwa wakati.

‎Amesema serikali itaendelea kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto kwa kuzingatia miongozo na ushahidi wa kisayansi, kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kuboresha huduma wakati na baada ya kujifungua, pamoja na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuanza kliniki mapema na kupata huduma stahiki.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!