Latest Posts

WAFANYABIASHARA IRINGA WAHIMIZA WENZAO KUDAI RISITI NA KULIPA KODI KWA WAKATI

Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Iringa wameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuendelea kutoa huduma nzuri pamoja na elimu ya kodi, wakisema hatua hiyo imewasaidia kuelewa kwa kina zaidi wajibu wao wa kikodi na umuhimu wa kuzingatia sheria na taratibu katika shughuli zao za biashara.

Wafanyabiashara hao wametoa pongezi hizo baada ya kutembelewa na maafisa wa TRA Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Meneja wa TRA wa Mkoa huo Maigloria Saria, katika ziara yenye lengo la kuwafikia wafanyabiashara katika maeneo yao na kuwapa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kodi.

Wamesema ziara hiyo imekuwa na manufaa kwa kuwa imewapa fursa ya kuuliza maswali na kupata majibu ya moja kwa moja kuhusu changamoto na masuala mbalimbali yanayohusu kodi na uendeshaji wa biashara kwa kuzingatia sheria.

Aidha, wafanyabiashara hao wamewahimiza wenzao pamoja na wananchi kwa ujumla kuendelea kudai risiti kila wanapofanya manunuzi, wakieleza kuwa kudai risiti ni sehemu muhimu ya kuimarisha utii wa sheria za kodi na kuchangia katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Wamesisitiza pia umuhimu wa wafanyabiashara kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati kabla ya tarehe 30, 2026, huku wakieleza kuwa ushirikiano mzuri kati ya TRA na wafanyabiashara ni msingi muhimu wa kujenga uelewa na kuimarisha mazingira ya biashara.

Aidha wafanyabiashara hao wameishukuru TRA Mkoa wa Iringa kwa kuendelea kuwafikia katika maeneo yao ya biashara, wakisema hatua hiyo imekuwa chachu ya kuongeza uelewa kuhusu ulipaji wa kodi, haki na wajibu wa mlipakodi pamoja na umuhimu wa kufuata sheria.

Wamewataka wafanyabiashara wengine kuendelea kushirikiana na TRA, kutoa taarifa na kufuata taratibu za kikodi, wakieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kukuza biashara zao na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Miongoni mwa wafanyabiashara waliotembelewa ni Asas Real Estate Limited, Patriot Hardware Limited, Iringa Food and Logistics Limited pamoja na Premier Product Co. Limited.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!