Latest Posts

MUCE KUANZISHA KOZI 7 ZA UZAMILI MWAKA 2025/2026 KUFUATIA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU

Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), kimeanzisha rasmi kozi saba za uzamili kwa mwaka wa masomo 2025/2026, hatua inayotokana na uboreshaji mkubwa wa miundombinu katika chuo hicho, hususan ujenzi wa maabara za kisasa za sayansi na mabweni ya wanafunzi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Rasi , Taaluma , utafiti na ushauri elekezi wa chuo hicho, Prof. Deudedit Rwehumbiza , amesema kati ya kozi hizo mbili ni za umahiri (Master’s degree programmes) na tano ni za uzamivu (PhD programmes) ambazo zimeundwa kutokana na mahitaji halisi ya jamii katika nyanja mbalimbali.

“Kozi hizi zinalenga kujibu changamoto za kijamii kupitia tafiti na tafsiri ya nadharia katika vitendo. Tumejipambanua kama taasisi ya elimu ya juu inayozingatia sayansi na maendeleo ya jamii,” amesema Prof. Rwehumbiza .

Prof. Rwehumbiza ameishukuru serikali kwa kufanikisha uboreshaji wa miundombinu kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), ambapo zaidi ya Shilingi bilioni 14 zimetumika kujenga maabara za sayansi na mabweni ya kisasa kwa ajili ya wanafunzi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shahada za Uzamili wa chuo hicho, Chacha Steven Chacha, amesema MUCE imejipanga kutoa elimu bora yenye kukidhi mahitaji ya soko la ajira, huku ikiwajengea wanafunzi uwezo wa kutatua matatizo halisi ya kijamii na kisayansi.

Kozi hizo mpya zinatarajiwa kuanza rasmi mwaka wa masomo 2025/2026, hatua inayotajwa kuwa chachu ya kuimarisha mchango wa MUCE katika maendeleo ya kitaifa kupitia elimu ya juu na utafiti.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!