Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amezindua duka la mkaa rafiki eneo la Nzuguni Jijini Dodoma lenye lengo la kuhakikisha kila Mtanzania anapika kwa Nishati safi na kulinda afya na mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo hasa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia, lengo ni kuhakikisha takribani asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.
Uzinduzi wa duka hilo umefanyika leo Jumatatu Juni 24,2025 kwa kusimamiwa na Shirika la Madini Taifa  (STAMICO) pamoja na Shirika lisilo la kiserikali Foundation for Disabilities Hope.
RC Senyamule amesema Kati ya makundi unayoathirika na nishati isiyo safi mojawapo ni kundi la watu wenye ulemavu wa ngozi hivyo duka hilo litakuwa nisehemu ya utatuzi wa Changamoto yao.