Latest Posts

REAL MADRID YAWASILISHA USHAHIDI UEFA SAKATA LA UBAGUZI

Na SHABIH KASSIM

Klabu ya Real Madrid imetangaza kuwa imewasilisha ushahidi wote uliopo kwa UEFA kuhusiana na matukio ya ubaguzi wa rangi yaliyotokea wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa wiki iliyopita mjini Lisbon dhidi ya SL Benfica.

Kupitia taarifa yake rasmi, Real Madrid imeeleza kuwa imeshirikiana kikamilifu na uchunguzi ulioanzishwa na UEFA kufuatia vitendo hivyo visivyokubalika, ambavyo vilimhusu mchezaji wake, Vinícius Júnior. Klabu hiyo imeweka wazi kuwa inachukulia suala la ubaguzi kwa uzito mkubwa na iko tayari kutoa ushirikiano wowote unaohitajika.

Real Madrid pia imewashukuru wadau wa soka duniani kwa mshikamano, sapoti na upendo mkubwa uliotolewa kwa Vinícius Júnior baada ya tukio hilo, ikisisitiza kuwa ujumbe huo wa pamoja unaonesha wazi msimamo wa jamii ya soka dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Klabu hiyo imesisitiza kuwa itaendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi zote husika kupambana na ubaguzi wa rangi, vurugu na chuki katika michezo na jamii kwa ujumla, ikilenga kuhakikisha soka linabaki kuwa mchezo wa heshima, usawa na mshikamano kwa wote.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!