Latest Posts

SERIKALI YAAGIZA SHULE ZOTE ZIFUNGWE NOVEMBA 13 KISA EL NIÑO

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa Waraka wa Elimu Na. 3 wa Mwaka 2026 unaoelekeza shule zote za awali, msingi na sekondari nchini Tanzania Bara kufungwa mapema tarehe 13 Novemba 2026 badala ya tarehe 4 Desemba 2026 kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Umauzi huo umechukuliwa kama hatua ya tahadhari baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kutoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za vuli kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2026, ikionya kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa za El Niño zinazoweza kusababisha mafuriko na athari nyingine katika baadhi ya maeneo.

Waraka huo rasmi uliotolewa tarehe 30 Septemba 2026 wenye Kumbukumbu Namba CA.128/191/01J/53 na kusainiwa na Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene M. Mtahabwa umeeleza kuwa, “Kwa kuwa madhara ya mvua za El Nino yanaweza kuathiri shughuli za uendeshaji wa shule kwa ujumla ikiwa ni pamoja na wanafunzi wasio katika madarasa ya Upimaji na Mitihani ya Kitaifa, ni muhimu kuchukua hatua za tahadhari kwa ajili ya usalama na ustawi wa wanafunzi wote, walimu na watumishi wengine katika shule”.

Mabadiliko haya ya tarehe za kufunga shule yamebadilisha maelekezo ya awali yaliyokuwa katika Waraka wa Elimu Namba 06 wa Mwaka 2025 kuhusu kalenda ya mihula ya masomo kwa shule za awali, msingi na sekondari kwa mwaka 2026, pamoja na Waraka wa Elimu Namba 01 wa Mwaka 2026 uliokuwa ukielekeza kufungwa kwa shule tarehe 4 Desemba 2026

Uamuzi huu unajiri kufuatia hatua ya awali iliyochukuliwa na Wizara tarehe 25 Septemba 2026 ya kubadili tarehe za Upimaji na Mitihani ya Kitaifa ili kuepuka usumbufu unaoweza kusababishwa na mafuriko hayo. Waraka huu mpya umeanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 1 Oktoba 2026.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!