Latest Posts

TANESCO PWANI: UKIONA DALILI ZA WIZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME TOA TAARIFA POLISI

Meneja wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Pwani Mhandisi Cosmas Mkaka ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Pwani kuwa mstari wa mbele kulinda na kutoa taarifa za wananchi wanaojihusisha na vitendo vya wizi wa miundombinu ya umeme mkoani humo kwani husababisha kukatika kwa umeme na kusababisha hasara kwa TANESCO.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kuhusu changamoto ya wizi wa miundombinu ya umeme mkoani Pwani ambapo amesema wizi huo husababisha shirika hilo kuingia gharama ya kurejesha miundombinu hiyo ili wananchi wapate umeme.

“Najua tumeshaongea na viongozi wa Serikali za Mitaa vijiji na madiwani lakini niombe na wananchi wengine wote, ukiona kuna dalili zozote zinazoweza kuharibu miundombinu wasisite kuwasiliana na uongozi wa Kijiji husika, vituo vya polisi au hata kutupigia simu tuweze kuokoa mali ambayo ingeweza kuibiwa au kuharibiwa na tukapata hasara kubwa” Amesema Mhandisi Mkaka.

Aidha Mkaka amewashukuru wananchi walioonesha ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbali za usalama wa miundombinu ya shirika hilo.

“TANESCO ni shirika la serikali, la umma, la wananchi hivyo kinachoharibiwa ni cha kwetu sote, tukiwajibika kulinda miundombinu yetu ambayo ni mali yetu sote, itatusaidia sisi sote kuwa na maendeleo katika mkoa wetu wa Pwani hivyo tusaidiane kwani inavyoharibiwa inaharibu kodi za wananchi” Alisema Mkaka.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!