Tanzania imeshiriki kikamilifu katika Jukwaa la Biashara kati ya Nchi za Afrika na Urusi, lililofanyika tarehe 9 Novemba 2024, mjini Sochi, Urusi, kupitia ujumbe wake ulioongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dennis Londo.
Â
Kongamano hilo lilikuwa na kauli mbiu ya “Kuimarisha Ushirikiano wa Kibiashara kati ya Urusi na Nchi za Afrika”, na liliongozwa na Dkt. Binilith Mahenge, Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Â
Lengo kuu la kongamano lilikuwa ni kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo barani Afrika, huku Tanzania ikiwa ni kivutio kikuu kutokana na fursa zake katika sekta mbalimbali, kama vile nishati, kilimo, na teknolojia.
Â
Katika kongamano hilo, washiriki kutoka Tanzania walijitokeza kutangaza fursa za kipekee zinazopatikana nchini kwa wawekezaji wa kimataifa.
Â
Jukwaa hili lilikuwa ni fursa muhimu kwa Tanzania kukuza ushirikiano wa kibiashara na Urusi, na kutoa jukwaa kwa wawekezaji kuonesha nia yao ya kuwekeza katika maeneo ya kimkakati yanayohitaji msaada na ushirikiano wa kimataifa.