Latest Posts

TLS YAUNDA KAMATI KUCHUNGUZA MGOGORO WA NGORONGORO

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Boniface Mwabukusi amesema Baraza la Uongozi la chama hicho limeunda kamati maalumu kufuatilia suala la Ngorongoro ili kujua ukweli wake.

Mwabukusi amezungumza hayo alipokutana na wanahabari Jumanne Agosti 20, 2024 ambapo amesema pamoja na kufuatilia suala hilo kamati hiyo litafanya kazi zifuatazo;

(I) Kufanya mashauriano na taasisi mbalimbali pamoja na kutembelea baadhi ya maeneo yenye migogoro ili kujua uhalisia wa migogoro husika

(ii) Kufanya mapitio ya sera, sheria na mazoea pamoja na kuzichambua kuhusiana na umiliki wa ardhi kwa wazawa pamoja na shughuli za uwekezaji na uhifadhi na kubaini uzingativu wa haki za msingi za raia katika maeneo husika kwa kuzingatia Katiba, sera na sheria za nchi

(iii) Kuandaa kongamano (Symposium) la kitaifa kuhusiana na namna bora ya kufanya maendeleo kwa kuzingatia na kulinda haki za wazawa katika ardhi zao za asili pamoja na haki zao za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni katika maeneo yanayofikiwa na shughuli za uwekezaji

(iv) Kubaini mashauri au hatua zote ambazo zimechukuliwa na walalamikaji pamoja na walalamikiwa kisheria na kiutaratibu katika kuhakikisha uzingativu wa sheria na kubaini majina ya watu ambao kweli wameridhia kuondoka kwa hiyari kwenye maeneo yao na ambao hawakuridhia kuondoka kwa hiyari kwa sababu ya wao kuamua kubaki katika eneo lao la asili Ngorongoro

(v) Kubaini na kulishauri Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika TLS) juu ya hatua zakuchua ili kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu suala la migogoro ya ardhi inayosababishwa na mipango ya uwekezaji au uhifadhi

Kamati hiyo itafanya kazi ndani ya siku 30 kuanzia Agosti 21.2024.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!