Latest Posts

UMOJA WA AMANI KWANZA KAGERA WAKEMEA VITENDO VYA UKATIRI DHIDI YA WAZEE

Theophilida Felician Kagera.

Wito huo umetolewa naye mwenyekiti wa taasisi hiyo Mauldi Rashidi Kambuga akiungana na wadau wa kundi la Kagera mpya nakwenda kuwafariji wazee wanaolelewa kituo cha Kiilima kilichopo kata Nyakato Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera.

Mwenyekiti Kambuga awali ameanza kuwatia moyo wazee hao akisisitiza kwamba wazee ni hazina na nikundi muhimu sana kwa jamii hivyo wanahitaji kuthaminiwa, kupendwa, faraja na mengineyo mengi ili kuwasadia kuishi vizuri kama ilivyo kwa makundi mengine.

Amesema kwamba wazee mara kadhaa hukabiliwa na madhira mbalimbali yakiwemo ya ukatiri wa mauaji hivyo yapaswa kila mmoja kuyakemea kwa nguvu zote maovu hayo.

Amewapongeza waliowaza nakuandaa zoezi hilo la kuwafikia wazee wa kilima huku akifafanua kwamba taasisi ya umoja wa amani kwanza baada ya kukabidhiwa wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee wanawake na watoto kutoka wizara ya mambo ya ndani imepata nguvu mpya yakuifikia jamii kwa kushiriki mambo tofauti tofauti likiwemo suala nyeti la kuhamasisha namna yakuitunza amani.

Viongozi wa dini sheikh Mussa Hassan pamoja naye Jovestus Sebastian katika dua wameelezea na kuhimiza jinsi wazee wanavyohitaji faraja ya kutunzwa vizuri hatimaye kuishi kwa neema badala ya kukatishwa tamaa kama ambavyo imekuwa ikijitokeza kwa baadhi ya wazee.

Mkuu wa mkoa Kagera Mhe Hajat Fatma Mwassa akiwa mgeni rasmi wakati akizikabidhi zawadi hizo kwa wazee ambazo ni nguo aina mbalimbali, sukari, mchele, unga, sabuni na viti mwendo amewapongeza wale wote kutoka kundi la Kagera mpya wakiongozwa na Jastin Kimodoi anayeishi Marekani aliyechochea jambo hilo kwa wenzake hadi likafanikiwa vyema.

Aidha ameipongeza taasisi ya umoja wa amani kwanza nchini na mkoa kwa ujumla kwa namna ilivyojiimarisha kuifikia jamii na kuitangaza injili ya amani kwani amani ndiyo inayowezesha kufanyika kwa kila jambo.

Mzee Wilison Habyalimana ni balozi wa wazee kituoni hapo kwaniaba ya wazee wenzake ameshukuru wadau hao kwa ujio wao huku akiitaja changamoto kubwa ya uhaba wa maji ambapo mkuu wa mkoa Fatma Mwassa amewahidi juhudi zitafanyika mapema ili kujengwa kisima cha maji katika kituo hicho.

Naye mlezi wa kituo Gladness Lwiza amebainisha kuwa kituo hicho wapo wazee (19) wakiume (14) na wakike( 5) naye ameshukuru kwa dhati misaada hiyo ya wadau.

Baadhi ya wadau akiwemo Joseph Muzanila mtanzania anayeishi Marekani pia ameahidi kuwahamasisha watu wengine ili kukisaidia mahitaji ya muhimu kituo hicho cha wazee Kilima.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!