Latest Posts

WANAKIJIJI WAPATIWA ELIMU YA URASIMISHAJI WA ARDHI

Wananchi wa Kijiji cha Kware Kata ya Masama Kusini Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, wamepatiwa elimu juu ya umuhimu wa urasimishaji wa ardhi kama njia ya kuimarisha umiliki halali wa maeneo yao na kuongeza thamani ya ardhi wanayomiliki.

Elimu hiyo pia imelenga kupunguza migogoro ya ardhi katika jamii na kuweka msingi thabiti wa uwekezaji wa kisasa, ambapo zoezi la urasimishaji linatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akizungumza na kutoa taarifa katika Mkutano wa Kijiji Afisa Mtendaji wa kijiji hicho cha Kware, Edwine Lamtey amesema kuwa walipokea kiasi cha shilingi milioni 49.8 kutoka Serikali kuu,fedha zitakazotumika kutekeleza mradi wa usambazaji endelevu wa maji vijijini na usafi wa mazingira ambapo mradi huo utahusisha ujenzi wa miundombinu ya maji safi, vyoo bora, kichomea taka, pamoja na mashimo ya kutupia kondo la nyuma na majivu.

“Tayari tumepokea fedha hizi na kazi yangu kama msimamizi ni kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ubora unaotakiwa,kwa wakati na kwa kuzingatia thamani ya fedha ya umma,fedha hizo ni kwa matumizi maalum na hakutakuwa na uvumilivu kwa yeyote atakayekiuka taratibu.”alisema Lamtey.

Katika hatua hiyo amewataka wananchi wa Kijiji hicho kuchangamkia fursa ya kurasimisha maeneo yao ili yawe na tija na kuongezewa thamani wakati wa uuzaji au shughuli za uwekezaji.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Sabastian Kimaro, alisema kuwa mbali na fedha hizo, kijiji cha Kware pia kimepokea shilingi milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa madawati na milioni 3 kutoka mfuko wa jimbo kwa ajili ya ujenzi wa jiko la shule.

Sabrina Lema, mkazi wa kitongoji cha Boma Kati, ameeleza kuridhishwa na kasi ya maendeleo katika kijiji hicho kwa kipindi kifupi, ambapo kumekuwa na mabadiliko makubwa yanayoonyesha kuwa mshikamano kati ya wananchi na serikali ni silaha muhimu ya maendeleo ya kweli.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!