Watuhumiwa wanne wa kesi ya kumbaka na kumlawiti binti wa Yombo wamefikishwa mahakamani Agosti 19,2024 kufuatia video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha binti huyo akiingiliwa kinyume na maumbile na kikundi cha watu huku wakidai wametumwa na afande kufanya uovu huo.
Watuhumiwa hao wamefikishwa katika kituo jumuishi cha utoaji haki, Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma na kusomewa makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni kubaka kwa kundi na kosa la pili ni kumuingilia kinyume cha maumbile binti huyo.
Watuhumiwa hao ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo, Amin Lord Lema, Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Renatus Mkude, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, kesi hiyo itasikilizwa kwa siku tano kuanzia Agosti 19 hadi Agosti 23 siku ya Ijumaa.