Latest Posts

WAZIRI MAVUNDE AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUCHUKULIWA DHIDI YA WANAOCHELEWESHA MIRADI

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameagiza hatua za haraka kuchukuliwa dhidi ya wale wanaochelewesha miradi ya maendeleo kwa kutumia vibaya fedha za umma.

Akizungumza katika kijiji cha Ushirika, wilaya ya Mbogwe, Geita, amesisitiza umuhimu wa usimamizi bora wa rasilimali za umma wakati akiweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa hospitali iliyocheleweshwa kutokana na usimamizi dhaifu.

Serikali ilitenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya mradi huo, lakini imeongeza milioni 60 zaidi kutokana na ucheleweshaji.

Mavunde ameagiza zabuni ya ujenzi kutangazwa ndani ya wiki moja na kasoro zilizobainika, kama milango isiyokidhi viwango, zirekebishwe.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela, amethibitisha kuwa hatua za kinidhamu na kisheria zimeanza kuchukuliwa dhidi ya waliohusika kuchelewesha mradi.

Kwa upande wao wananchi, wameipongeza serikali kwa jitihada za kuboresha huduma za afya, wakibainisha kwamba awali walikosa huduma ya haraka, hususan kina mama wajawazito.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!