Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama Oktoba 5, 2024 akiwa katika ziara Mkoani Kilimanjaro amekagua Ujenzi wa Zahanati iliyopo katika kijiji cha Mawasiliano Jimbo la Siha pamoja na kuweka Jiwe la Msingi ambapo Zahanati hiyo itasaidia kupunguzia adha Wananchi kutembea mrefu wa Km 4 kupata huduma za Afya.
Waziri Mhagama ameielekeza Halmashauri ya Wilaya ya Siha kujenga kichomeo taka haraka pamoja na sehemu ya kupumzikia ndugu wa wagonjwa ili Zahanati hiyo ianze kufanya kazi ndani ya wiki moja Oktoba 12, 2024 kutoka Oktoba 5, 2024 alipotoa maagizo hayo.
Akizungumza mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Dancan Urassa amesema kuwa Zahanati hiyo itaenda kuwa mkombozi kwa Wananchi 3,000 kulingana na sensa ya watu 2022 hasa Jamii ya wafugaji waliopo maeneo hayo pamoja na Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari.
Zahanati hiyo imetumia gharama ya shilingi Milioni 93 hadi kukamilika ikiwemo mapato ya ndani ya Kijiji Milioni 28, Mapato ya ndani ya Halmashauri Milioni 15 na ruzuku kutoka Serikali kuu Milioni 50