Waziri wa afya nchini Kenya, Aden Duale amewataka wananchi kutokuwa na hofu kutokana na mripuko wa ugonjwa wa Eborla nchini humo, huku akisisitiza kuwa mifumo yote ya afya na vituo vya karantini nchini viko imara kukabiliana na kudhibiti kusambaa kwa mlipuko huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Nairobi siku ya leo Octoba 6,2026, Waziri wa Afya Aden Duale amethibitisha kutokea kwa kisa cha kwanza kabisa cha ugonjwa wa Ebola nchini humo, kikiambatana na kifo cha mgonjwa mmoja na kusababisha hofu kubwa ya kiafya kwa mamlaka na wananchi kwa ujumla
Kulingana na ripoti rasmi kutoka Wizara ya Afya ya Kenya inabainisha kuwa marehemu ni mwanamume raia wa Kenya ambaye amekuwa akiishi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa muda wa miaka saba iliyopita. Inaarifiwa kuwa mgonjwa huyo alianza kuonyesha dalili za ugonjwa huo takriban mwezi mmoja uliopita akiwa bado nchini DRC.

Taalilifa zinaeleza kuwa mgonjwa yuyo labla ya kurejea nchini Kenya alipataiwa matibabu katika hospitali kadhaa nchini Congo lakini hali yake bado ilizidi kudhoofika, ndipo alipo amua kusafiri kurejea nchini humo.
Hata hivyo, hali yake ilizidi kuzorota haraka baada ya kuwasili ambapo alionyesha dalili kuu za ugonjwa huo ikiwemo homa kali, mtetemo wa mwili, uchovu mwingi, kudhoofika kwa misuli, maumivu wakati wa kumeza chakula, na kuvuja kwa damu chini ya ngozi. Kutokana na hali hiyo, na kupelekwa kwa dharura katika Hospitali ya 4 ambako aliwekwa karantini.
Aidha vpimo vya maabara vilivyofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya (KEMRI) na Maabara ya Kitaifa ya Rejea ya Virusi vilihibitisha uwepo wa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo. Licha ya jitihada kubwa za madaktari za kumpatia matibabu, mgonjwa huyo anafariki dunia usiku wa Jumatatu, Oktoba 5, 2026.
Katika ripoti yake ya dharura, Shirika la Afya Duniani WHO linabainisha kuwa mlipuko huu wa virusi vya Bundibugyo umekuwa ukiongezeka kasi tangu katikati ya mwezi Mei nchini DRC, ukiwa umeshasababisha vifo vya zaidi ya watu 4,000 kati ya visa zaidi ya 8,400 vilivyothibitishwa. WHO inaeleza kuwa virusi hivi vya Bundibugyo havina chanjo au matibabu maalum yaliyopitishwa kisheria hadi sasa, jambo linalofanya ugonjwa huu kuwa hatari zaidi.
Kufuatia kifo hicho, Serikali inafanikiwa kuwatambua watu 28 waliokutana kwa karibu na marehemu, wakiwemo wanafamilia yake na wahudumu wa afya. Wakati huo huo, timu ya dharura ya afya inafanya kazi usiku na mchana kuwatafuta abiria wengine 23 na wahudumu wanne wa ndege waliokuwa safari moja na mgonjwa huyo kutoka Uganda.
Baada ya hali hiyo Serikali ya Kenya inashirikiana na wataalamu kutekeleza taratibu salama na za heshima za mazishi kwa mujibu wa itifaki za kimataifa ili kuzuia maambukizi zaidi.