Latest Posts

TIC WATOA SEMINA KATIKA SEKTA YA MAJI, UMEME, MAFUTA GESI NA MADINI

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimetoa semina ya miradi kati ya Tanzania na Korea kwa wakorea waliopo nchini na wengine mtandaoni.

Akizungumza wakati wa semina hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 24, 2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri amesema kuwa semina hiyo ina lengo la kuimarisha uhusiano wa kibishara na kubadilishana taarifa na kushirikiana katika sekta muhimu za maji, umeme, mafuta, gesi na madini.

Teri amesema kuwa semina hiyo imehusisha ujumbe mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi, ya Korea kukiwa na kampuni zaidi ya 38 za Korea na za biashara 50 za Tanzania ambazo zimeonesha nia ya kushirikiana pamoja katika masuala ya uwekezaji na biashara.

“Kuanzia mwaka 1997 hadi Septemba 2024 Korea, kupitia TIC, imesajili miradi yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 89.94 (USD) ikiwa na miradi 68 na kutoa ajira 4,997” amesema Teri.

Amesema Semina hiyo ilikuwa jukwaa muhimu kwa wadau kutoka mataifa Korea na Tanzania ili kukuza ushirikiano unaoweza kuharakisha ukuaji wa uchumi.

“Tunaweka msisitizo kwa majadiliano ya wazi kati ya maafisa wa serikali, viongozi wa biashara, na wataalam wa sekta mbalimbali ili kushughulikia mabadiliko ya sera na kuunda mazingira bora ya uwekezaji wa kigeni” amesema Teri.

Licha ya hayo Teri amewashukuru washiriki wote walioshiriki mtandaoni na waliofika katika ukumbi kwa ajili ya kushirikisha uzoefu wao na kujua fursa za uwekezaji ambazo Tanzania inatoa.

“Pamoja, tunaweza kujenga uhusiano wa kiuchumi endelevu ambao utawafaidisha Korea na Tanzania.” amesema Teri.

Semina hiyo imetolewa na TIC kwa kushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania, Shirika la Kukuza Uwekezaji wa Biashara la Korea (KOTRA), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Mfuko wa Sekta binafsi Tanzania (TPSF), na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA).

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!