Latest Posts

LUGANGIRA ASISITIZA UADILIFU BIMA YA AFYA KWA WOTE.

Bima ya Afya kwa Wote inalenga kulinda familia dhidi ya gharama kubwa za matibabu, kupunguza umasikini unaotokana na maradhi na kuhakikisha wananchi hawalazimiki kuuza mali zao au kukopa fedha ili kupata huduma za afya.

‎Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Kichiki Lugangira, wakati akizindua awamu ya pili ya Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote mkoani Arusha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, CPA Amos Gabriel Makalla, katika viwanja vya Field Force Unity (FFU), Kwa Mrombo, jijini Arusha, Oktoba 22, 2026.

‎

‎Lugangira amesisitiza kuwa mpango huo unapaswa kutekelezwa kwa uadilifu, uwazi na uwajibikaji ili kuwafikia wananchi wote, wakiwemo wakulima, wafugaji, wafanyabiashara wadogo, waendesha bodaboda, vijana, wazee na wanawake wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujipatia kipato.

‎Aidha, amewataka viongozi na watendaji kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya vinakuwa tayari kuwahudumia wananchi, mifumo ya udhibiti wa ndani inafanya kazi na malalamiko yanashughulikiwa kwa wakati nakuongeza kuwa mafanikio ya mpango huo hayatapimwa kwa idadi ya walioandikishwa pekee, bali pia kwa ubora wa huduma na upatikanaji wa matibabu yanayohitajika.

‎

‎Kwa upande wake, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Arusha, Hipoliti Lello, amesema Serikali imeweka kipaumbele kwa kaya zisizo na uwezo, ambapo mkoa huo umelenga kusajili kaya 29,334 zenye jumla ya wanufaika 80,909 ambao gharama za bima zao zitalipwa na Serikali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!