
Kituo cha michezo cha Suluhu Academy kutoka visiwani Zanzibar (Kizimkazi) kimesaini mkataba wa kushirkiana na taasisi ya Chato Samia Cup iliyoko wilaya ya Chato mkoani Geita kwaajili ya kuibua vipaji na kuviendeleza.
Tukio hilo limefanyika wakati wa mchezo wa ufunguzi wa ligi ya Chato Samia Cup 2024 iliofanyika kwenye uwanja wa Mazaina uliopo Chato mjini kati ya timu ya mashabiki wa Simba wilayani Chato dhidi ya Suluhu Sports Academy.
Tukio hilo pia limeshuhudiwa na Mhandisi Deusdedith Katwale ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya Chato Samia Cup ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Tabora.
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Mheshimiwa Martin shigella, mkuu wa Wilaya ya Geita Mheshimiwa Hashim Abdallah Komba amewaasa viongozi na wadau wa michezo wilayani Chato kutumia fursa hiyo kuonesha ushirikiano ili kuendelealza michezo kwani ni moja ya jitihada za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta ya michezo nchini.
Aidha Komba amewatakabviongozi hao kuacha kuihusisha Chato Samia Cup na hisia nyingine ..
“Vipaji vinavyoibuliiwa hapa ni kwa faida Chato, mkoa na Taifa kwa ujumla, oneni dhamira njema ya Chato Samia Cup na isiwekewe hisia hisia nyingine maaana ni kukwamisha vipaji vilivyopo kwenye maeneo yenu, turuhusu shughuli za maendeleo zifanyike badala ya kuweka hofu na kutaka kukwamisha” Mheshimiwa Komba, Mkuu wa Wilaya ya Geita.
Naye katibu wa Chama cha Soka wilayani Chato (CDFA) Wilfred Machugu ambaye ameshiriki zoezi la kusaini mkataba amekiri kuwa mkataba huo ni msaada mkubwa kwa chama cha soka pamoja na wadau wa michezo Kkwani itawasaidia kuwaendeleza vijana waowapata kupitia ligi ya Chato Samia Cup na mashindano mengine kuwapeleka kwenye kituo cha michezo cha Suluhu Academy kwaajili ya kujiendeleza zaidi.
Kwa upande wao baadhi ya wachezaji kutoka wilayani Chato wameishukurua taasisi ya Chato Samia Cup kwa kuwaleta Suluhu Sports Academy wilayani hapo kwani hatua hiyo imeongezea hamasa ya vijana kuonesha uwezo wao Ili waweze kuonekana na kuendelezwa zaidi .
Zoezi la kusaini mkataba huo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na kisiasa akiwemo mwazilishi wa ligi ya Chato Samia Cup Deusdedith katwale ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Tabora.
Huu ni msimu wa pili wa ligi ya Chato Samia Cup kufanyika ambapo baada ya uzinduzi huo ligi hiyo itaendelea kwa ngazi ya chini kuanzia vijijini ambapo zaidi ya timu 100 zinatarajiwa kushiriki Ili kumpata bingwa ambaye atajinyakulia kombe na zawadi ya shilingi milioni mbili .