Latest Posts

KIGOMA YAPEWA PONGEZI KWA UMAHIRI WA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA

Watendaji wa serikali mkoani Kigoma wametakiwa kuzingatia miongozo ya matumizi ya fedha za umma ili kufanikisha mipango ya serikali inayolenga kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Hassan Rugwa, baada ya mkoa huo kushika nafasi ya tatu katika kipengele cha mikoa kwenye Tuzo za Umahiri wa Uandaaji wa Hesabu za Fedha kwa mwaka 2022/2023.

Tuzo hizo, zinazoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), zinalenga kutambua taasisi zinazozingatia viwango vya kimataifa vya uhasibu. Rugwa amewapongeza watendaji wote wa mkoa kwa ushirikiano wao uliowezesha Kigoma kuendelea kuwa miongoni mwa mikoa bora kwa kipindi cha miaka sita mfululizo.

“Kwetu tuzo hii inatoa tafsiri pana na kuonesha kuwa tunatekeleza majukumu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Matumizi ya Fedha kuanzia upangaji wa bajeti na mlolongo wa utekelezaji wa bajeti hiyo katika mkoa na mamlaka za Serikali za Mitaa” amesisitiza Rugwa.

Aidha, Rugwa amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma za jamii mkoani Kigoma, hatua inayoongeza fursa za kiuchumi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zaidi.

Kwa upande wake, Muhasibu Mkuu wa Mkoa, Johnson Gamba, amesema mkoa umeendelea kupata tuzo hiyo kwa miaka sita ikiwa ni ishara ya uongozi wa mkoa wa Kigoma kusimamia vizuri fedha zinazotolewa na serikali katika kutekeleza kazi na miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Ni vizuri watendaji wote tunaohusika na matumizi ya fedha ngazi ya mkoa na halmashauri kuhakikisha tunaendelea kuimarisha na kuzingatia mifumo ya ndani ya usimamizi na matumzi ya fedha za umma”, amesema Gamba.

Aidha, amewataka wakuu wa idara na vitengo kuwajengea uwezo watendaji walio chini yao ili waweze kuelewa na kufuata miongozo ya matumizi ya fedha za umma kwa ufanisi zaidi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!