Latest Posts

WANAJESHI 75 WA CONGO KUHUKUMIWA KWA KUKIMBIA MAPIGANO DHIDI YA M23

Mamlaka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa wanajeshi wasiopungua 75 watahukumiwa siku ya Jumatatu kwa tuhuma za kukimbia vita dhidi ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, katika eneo la Kivu Kusini.

Wanajeshi hao wanatuhumiwa pia kwa kusababisha vurugu dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na mauaji na uporaji, kulingana na taarifa ya ofisi ya mwendesha mashtaka wa kijeshi iliyotolewa Jumapili.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imebaini ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanyika tangu M23 ilipoingia mashariki mwa Congo mwishoni mwa Januari na kuteka mji wa Goma. Kati ya vitendo vilivyoripotiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji wa genge na utumwa wa kingono. Ripoti hiyo inawataja waasi wa M23, wanajeshi wa Congo na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali kuwa wahusika wa vitendo hivyo.

Serikali ya Congo haijatoa maoni rasmi kuhusu ripoti zinazoihusisha na ukiukaji wa haki, lakini imeiomba Umoja wa Mataifa kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na M23 na Rwanda.

Hata hivyo, Rwanda imekanusha kuhusika katika mzozo huo, huku waasi wa M23 wakiwa bado hawajatoa tamko lolote kuhusu tuhuma hizo.

Licha ya M23 kutangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja, kundi hilo linaendelea kusonga mbele kuelekea kusini, likikaribia mji mkuu wa Kivu Kusini, Bukavu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!