Latest Posts

MAOMBI YA TAIFA YAIBUA WITO WA KUDUMISHA AMANI NA UMOJA

Serikali imeendelea kuhimiza maridhiano katika nyanja mbalimbali za kijamii na kisiasa ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa. Baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo nchini wamesema hatua hiyo inachangia kudumisha utulivu na kuweka mazingira wezeshi ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumza mkoani Morogoro katika kongamano la kuliombea Taifa amani, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Dkt. Eveline Munisi amesema amani na mshikamano ni nguzo muhimu zinazowezesha maendeleo endelevu, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuendelea kuvilinda na kuvidumisha.

Kwa upande wake, Nabii Joshua Mwantyala amesema viongozi wa dini wataendelea kuhubiri na kuhamasisha amani, upendo na maridhiano ili Tanzania iendelee kuwa Taifa lenye utulivu, umoja na maendeleo.

Naye Bishop Dkt. Willy Ackyoo pamoja na Bishop Daniel Ouma wameungana na waumini wa Kanisa la Sauti ya Uponyaji lililopo Manispaa ya Morogoro katika maombi maalumu ya kuliombea Taifa, wakisisitiza kuwa umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania ni msingi muhimu wa kudumisha amani, utulivu na maendeleo ya nchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!