Latest Posts

SHAHIDI ALIVYOBANANISHWA LISSU KUCHAPISHA VIDEO YOUTUBE YA JAMBO TV

Katika mwendelezo wa maswali ya dodoso kwa ACP Amini Mahamba katika shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Tundu Lissu, shahidi amedai kuwa mshtakiwa ndiye aliyechapisha video katika YouTube ya Jambo TV.

Shahidi huyo wa 16 katika kesi hii ya uhaini wakati akitoa ushahidi wake wa awali jana Agosti 10 aliieleza Mahakama kuwa alipewa jukumu la kusimamia na kuratibu upelelezi wa jalada la uhaini lililokuwa katiak ofisi ya Naibu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum Dar es Salaam.

Leo akihojiwa maswali hayo ya Dodoso ACP Mahamba amekiri kuwa katika maelezo ya mashahidi wengine katika kesi hiyo akiwemo P na P1 walikiri kuchapisha maudhui hayo.

Haya hapa maswali ya dodoso ya Lissu na majibu ya shahidi.

Lissu: Wewe si ndiye uliyesema nimechapisha hiyo video mtandaoni?

Shahidi: Ni mimi.

Lissu: Unafahamu maana ya neno kuchapisha mtandaoni?

Shahidi: Naifahamu.

Lissu: (Akisoma tafsiri hiyo kwenye sheria ya makosa ya mtandao) kuchapisha maana yake ni kusambaza, waeleze majaji kama mimi ndiye niliyesambaza video kwenye Youtube ya Jambo TV.

Shahidi: Ni wewe.

Lissu: Kuchapisha maana yake ni ‘transmitting’ waeleze majaji kama ni ushahidi wako kwamba mimi ndiye ‘niliyetransmitt’ hiyo video kwenye mtandao wa Jambo TV.

Shahidi: ndiyo, ni wewe.

Lissu: Waeleze majaji mama mimi nili-disseminate (kuitoa) hiyo video na ku-circulate na ku-deliver.

Shahidi: Ni wewe.

Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mfanyakazi wa au Mkurugenzi au Mtumishi wa Jambo TV.

Shahidi: Sina uhakika

Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mpiga picha au mtangazaji wa Jambo TV.

Shahidi: Sina uhakika

Lissu: Waeleze majaji kama mimi nina access kwa maana ya kuwa na password (nywila) ya kuingia kwenye mtandao wa Jambo TV, Youtube.

Shahidi: Sina uhakika

Lissu alirejea maelezo ya mashahidi P na P1 ambayo waliyaandika wakiwa Dodoma ambapo mashahidi hao wamesema walirusha mubashara mkutano wa Lissu na watia nia uliofanyika makao makuu ya CHADEMA

Lissu: Na wewe ndiye ulikuwa mpelelezi mkuu wa kesi hii na huna uhakika na hayo yote tuendelee

Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba hiyo video mnayodai ni ya uhaini ni kweli au si kweli kwamba ilichukuliwa na mtu aitwae P1 mfanyakazi wa Jambo TV

Shahidi: kweli

Lissu: Waeleze majaji kama umesoma maelezo ya P1

Shahidi: Niliyasoma

Lissu: Kwenye maelezo ya P1 ambayo wewe unasema umeyasoma yameandika siku hiyo tulikuwa na kamera tatu na kompyuta moja kamera tulizokuwa nazo ni aina ya Sony NX na tulikuw tunarusha mubashara katika mtandao wa youtube kupitia channel yetu ya Jambo TV, hayo ni maneno yaliyopo kwenye maelezo ya shahidi P1

Shahidi: Ni kweli

Lissu: kwenye

Baada ya kufika kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa makosa ya jinai tulikutana na askari mmoja ndipo akamtaka P akabidhi kitunza kumbukumbu memory card chenye video ilyorekodiwa April 3, 2025 kwenye mkutano wa Lissu na watia nia wa CHADEMA

Shahidi: Ni kweli

Lissu: Waeleze majaji kama ni kweli au si kweli kuna maelezo ya shahidi P na umeyasoma

Shahidi: Nimeyasoma

Lissu: Kwenye maelezo ya P alisema kwamba yeye ndiye aliyekuwa anapiga picha na kurusha matangazo hayo mubashara kwa kutumia kamera yake Sonny NX

Shahidi: Kweli

Lissu: Kwa hiyo P ndiye alikuwa anapiga picha na kurusha live

Shahidi: Ndio

Lissu: Waeleze Majaji kama ulienda kuhoji Makao Makuu CHADEMA Mkurugenzi ea habari ni nani mlimhoji Katibu Mkuu wa chama

Shahidi: Hapana

Lissu: Waeleze majaji kama mlimhoji Katibu Mkuu wa chama Golugwa

Shahidi: Hapana

Lissu: Waeleze majaji kama mlimhoji Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA amekaa hapo

Shahidi: Hapana

Lissu: Waeleze majaji kama mlimhoji mtu yoyote wa CHADEMA kuhusu mwaliko

Shahidi: Hao uliowataka

Lissu: Je mimi Mwenyekiti wa CHADEMA nawajibika kijinai kwa makosa yanayofanywa na viongozi wenzangu

Shahidi: Hauwajibiki

Lissu: Waeleze majaji kama ni kweli au si kweli kwamba hotuba yangu ilikuwa inahusu masuala ya Uchaguzi Mkuu na matatizo yake

Shahidi: ndiyo

Lissu: Kwa ushahidi wako umesema kwamba masuala ya uchaguzi  ni masuala yaliyopo kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi sasa naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji kama kwenye katiba hii ya nchi kuna mahali popote panaposema kwamba mtu anayetaka kuvuruga uchaguzi anayehamasisha kuvuruga uchaguzi usifanyike kafanya kosa la uhaini

Shahidi: Katiba haijaainisha hilo kosa.

Lissu: Waeleze majaji kama kwenye sheria ya uchaguzi  kuna kosa la jinai la kuvuruga uchaguzi

Shahidi: Sina uhakika sana

Lissu: Mimi nina uhakika sheria ya Uchaguzi wa Rais, Madiwani na Wabunge haina kosa lolote linaloitwa kuvuruga uchaguzi sio kosa lolote

Shahidi: Sheria zipo nyingi

Lissu: Twende kweye kanuni ya adhabu Uliulizwa kifungu ambacho nimeshtakiwa nacho ukasema ni kufungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu

Shahidi:(shahidi akakisoma)

Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba hicho kifungi kinazungumzia mtu anayetishia serikali bunge au mahakama na kikadhirisha anaechapisha ndiye anafanya kosa la uhaini

Shahidi: Ndio

Lissu: Nilitishia bunge au sikutisha

Shahidi: Ulitishia serikali

Lissu: Akiisoma hati ya mashtaka ikieleza kosa la uhaini na kumuuliza shahidi kama ni kweli au si kweli

Shahidi: Kweli

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama unafahamu maana ya neno serikali

Shahidi: Nafahamu

Lissu: Serikali maana yake ni nini

Shahidi: Ni mamlaka inayoendesha nchi ikiongoza nchi ikisaidiwa na mihimili yake mikuu mitatu, mhimili wa Utendaji, mhimili wa Mahakama na mhimili wa Bunge

Lissu: Hiyo ni kwa mujibu wa kitu gani

Shahidi: Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Lissu: )Akirejea Ibara ya 151(1) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

Swali la kwanza kwenye hayo maneno niliyosema waeleze majaji kama nimetaja neno serikali ya Jamhuri ya Muungano

Shahidi: hapana

Lissu: Waeleze majaji kama nimetaja serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Shahidi: Hapana

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama nimetaja Halmashauri ya jiji lolote la nchi hii

Shahidi: Haujataja

Lissu: Waeleze kama nimetaja jina la Rais wa nchi hii Samia Suluhu Hassan

Shahidi: Haujataja lakini ni sehemu ya Serikali

Lissu: Waeleze Majaji kama nimetaja jina la Philip Isdor Mpango

Shahidi: Hukutaja lakini sehemu ya Serikali

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama nilimtaja aliyekuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Shahidi: Haujataja lakini ni sehemu ya serkkali

Lissu: Waeleze Majaji kama kwenye hayo maelezo ya Uhaini nimetaja Tume ya uchaguzi

Shahidi: Haipo

Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba huyu Assistant Inspekta Andrew ndiye alichukua ushahidi kutoka kwa P na P1 kuuleta Dar es Salaam

Shahidi: Kweli

Lissu: Waeleze majaji kama umesoma maelezo ya Afisa wa Polisi Andrew Churu

Shahidi: Nimeyasoma

Lissu: Waeleze Majaji mnanitesea mimi nini wakati mna ushahidi wa waliorusha hayo

Shahidi: Nimeshalijibu

Lissu: Umejibuje

Shahidi: Jukumu langu kama mpelelezi ni kuthibitisha kosa la mshtakiwa

Lissu: Mnanitesea mimi nini

Shahidi: Huteswi

Lissu: Mwaka mmoja na miezi minne gerezani sio mateso

Maswali ya dodoso kwa shahidi bado yanaendelea Lissu akiendelea kuhoji zaidi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!