Latest Posts

RC MTAKA: NJOMBE TUNA WATOTO 3001 HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amewaagiza viongozi wa halmashauri zote mkoani humo kuanzisha kambi maalum za kuwafundisha wanafunzi 3,001 wa darasa la kwanza hadi la tatu ambao bado hawajamudu stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu.

Mtaka ametoa agizo hilo wakati akifungua kikao kazi cha maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Jifunze Kijiji Changu unaofadhiliwa na Taasisi ya Uwezo Tanzania, kilichofanyika mkoani Njombe.

Amesema kila kiongozi katika halmashauri ana wajibu wa kuhakikisha madarasa maalum yanaanzishwa kwa ajili ya wanafunzi hao, yakiwemo madarasa ya muda wa jioni, ili kuwapa fursa ya kujengewa uwezo katika stadi hizo muhimu.

Mtaka ameeleza kuwa mfumo huo unaweza kuendeshwa kwa utaratibu unaofanana na madarasa yanayoandaliwa kwa ajili ya mitihani, akisisitiza kuwa suala la wanafunzi kushindwa kusoma, kuandika na kuhesabu linahitaji hatua za haraka na za pamoja.

Kwa upande wake, Ofisa Elimu Mkoa wa Njombe, Nelas Mulungu, amesema Mradi wa Jifunze Kijiji Changu hautawahusu wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu pekee, bali pia utawajumuisha watoto ambao hawajawahi kwenda shule lakini wanaishi katika vijiji vinavyotekeleza mradi huo.

Naye Ofisa kutoka Uwezo Tanzania, Judith Kimambo, amesema wamefika mkoani Njombe kwa ajili ya kuuzindua mradi huo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha Watanzania wanapata stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!