Katika mwendelezo wa maswali ya Dodoso ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye shauri la uhaini linalomkabili ambalo linaendelea Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam mbele ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru Lissu amehoji kwa nini hakutafutwa kuulizwa maana ya maneno ambayo ameshtakiwa kwayo.
Lissu amemhoji shahidi wa 16 kwa mashahidi wa Jamhuri ACP Amini Mahamba ambaye alikuwa kiongozi wa timu ya upelelezi iliyopeleleza jalada la uhaini la Lissu lakini pia akiwa mpelelezi kwenye matukio ya Oktoba 29, 2025.
Lissu: Waeleze Majaji kama ulidhamiria maelezo yako ya kizimbani ya juzi yaaminiwe na mahakama kama ushahidi wa kweli
Shahidi: Nilidhamiria yatumike
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama maelezo yako uliyoandika polisi ulidhamiria yatumike mahakamani kama ushahidi wa kweli
Shahidi: Nilidhamiria yatumike
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kuna mahali popote umeelezea sababu ya hizo tofauti kati ya ulichoandika na ulichosema mahakamani
Shahidi: Hakuna mahali nilipoelezea
Lissu: Ushahidi wako kuhusiana na wale mashahidi waliofichwa mliowatoa mikoani unakumbuka ulisema kwamba hao mashahidi waliofichwa ni watu ambao walikamatwa na Polisi kweli si kweli
Shahidi: Kweli
Lissu: Na walikamatwa kwa kupanga njama za kufanya vurugu kwenye uchaguzi Mkuu
Shahidi: Walihamasisha
Lissu: Na walipokamatwa walikiri
Shahidi: Ndio
Lissu: Na waliandika maelezo yanayosema hivyo
Shahidi: Sahihi
Lissu: Hiyo mipango waliyokuwa wanaipanga ilikuwa makosa ya jinai
Shahidi: Kweli
Lissu: Wakakiri kwa maandishi, mkawaleta mahakamani wakakirri mahakamani au sio
Shahidi: Ndio
Lissu: Waeleze Majaji hizo tuhuma za kijinai mlizowakamata nazo ziliishia wapi
Shahidi: Nikirejea maelezo yangu baada ya kuwakamata baada ya kupata taarifa kutoka kwa maRCO tuliitisha jalada tukalisoma tukalipitia tulibaini wote walikuwa wamechochewa na wewe
Lissu: Ni kweli au si kweli mliwafutia kesi wote
Shahidi: walifutiwa
Lissu: Katika hao mashahidi walikuwepo waliotokea Dar es Salaam waeleze Majaji kama ni kweli au si kweli Dar es Salaam kulitokea vurugu zilizoua watu 182
Shahidi: Mimi sio Msemaji wa Jeshi la Polisi
Lissu: Kwa mujibu wa Tume ya Jaji Chande wstu 182 waliouawa Dar es Salaam kweli si kweli
Shahidi: Si kweli
Lissu: Mliwashtaki kwa makosa mlioowakamata
Shahidi:
Lissu: Umesema ulikuwa mpelelezi wa matukio ya Okt 29
Shahidi: Ndio
Lissu: Kuna watu mliwakamata Mbeya mkawaandika maelezo mkawaleta mahakamani halafu mkawaachia
Shahidi: Kweli
Lissu:Waeleze waheshimiwa majaji kama hiyo mikoa mitatu Dar es Salaam Arusha Mbeya jumla ya watu walioawa ni watu 315 kama kuna RPC, ZPC, RCO, OCD, OCCID au Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya aliyechukiliwa hatua kwa uzembe
Shahidi: Sina uhakika
Lissu: Waulize majaji kama wale waliosema wataenda kufanya vurugu na wakafanya kama kuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua mpaka sasa.
Shahidi: Ni matukio mawili tofauti
Lissu: Kuna mikoa mingine nane Mkoa wa Mwanza hawakukuletea taarifa kwamba kuna shida inapangwa kwenye uchaguzi
Shahidi: Sikupata
Lissu: Mwanza Okt 29 kwa mujibu wa Ripoti ya Jaji Chande waliuawa watu 90 waeleze majaji mwanza mna RPC
Shahidi:Â Ndio
Lissu: Kuna RCO, Mtu wa usalama wa taifa au mapolisi wote kama kuna aliyechukuliwa hatua kwa kutoona janga kubwa lililoukuta mkoa wa Mwanza
Shahidi: Sina uhakika
Lissu: Kwa Mikoa minne wameuawa watu 405 kwa mujibu wa Ripoti ya chande Songwe, Geita Mara, Shinyanga, Geita, Ruvuma katika mikoa hiyo ni Ruvuma pekee mlipewa taarifa kwamba watu wanapanga kufanya vurugu mkawakamata wakaandika maelezo ya mashtaka mkawaleta mahakamani mkawaachi ni kwel isi kwlei
Shahidi: Si kweli
Lissu: Kwa hiyo wa Songea mliwaleta mahakamani mkawashtaki
Shahidi: Waliachiwa kwa mujibu wa sheria
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama wote hawa vyombo vya ulinzi na usalama wamechukuliwa hatua yoyote
Shahidi: Sina uhakika
SHAHIDI ALIVYOULIZWA KAMA ALIZIONA VIDEO ZA KWENYE FLASH NA MEMORY CARD
Lissu: Je video mliyoangalia ikiwa mtandaoni au iliyokuwa kwneye Memory card iliyopokelewa dodoma au kwenye flash disc iliyoandikwa aldeepo
Shahidi: Iliyokuwa mtandaoni
Lissu: Kwa hiyo kwa jibu hilo ntakua sahihi hamkuangalia video ikiyokuwa kwenye memory card na ilyokuwa kwenye flash disc
Shahidi: Hatukuangalia
Lissu: Nitakuwa sahihi au nitakosea nikisema kwamba pengine kwenye hiyo flash disc aldeepo hakuna video yoyote
Shahidi: Sio sahihi
Lissu: Unajuaje wakati hukuangalia
Shahidi: Si kuna taarifa
Lissu: Unafahamu kama hata mahakamani hazikuletwa
Shahidi:
Lissu:Unajuaje kama hizo video zilikuwepo
Shahidi: Afisa wa polisi aliyekuwa anafanya upelelezi mtandaoni yeye ndiye alipakua hiyo video na kuweka kwenye flash. A/Insp Samwel Kaaya aliifanyia uchunguzi na kuilinganisha na video iliyorekodiwa na P na P1 baada ya uchunguzi aliandaa taarifa yake pamoja na ile video kwa ajili ya kuleta mahakamani kwa hiyo mpaka hivi sasa huo ushahidi upo kwa flash disc ambayo ina picha mjongeo zikizopakuliwa katika akaunti ya jambo TV na kuna ushahidi wa memory card iliyotumika kurekodi tukio hilo na taarifa ya uchunguzi ipo.
Lissu: Swali langu wewe unajuaje kama vipo wakati hukuziona
Shahidi: Nimefahamu kupitia taarifa ya mtaalamu wa uchunguzi
Lissu: Hiyo taarifa ipo Mahakamani? Mimi nina taarifa ilikataliwa kwa sababu haikuletwa na mtaalam
Shahidi:
Lissu: Mpaka sasa wewe ni shahidi wa 16 na nyie wote kuanzia shahidi wa kwanza mpaka wa 16 hakuna aliewasilisha ushahidi wa video taarifa ya uchunguzi nyaraka yoyote hakuna ushahidi pekee wa nyaraka uliopokelewa mahakamani ni uliowakilishwa kwa niaba yangu D1-D15 upande wa mashtaka hamjaleta chochote waeleze majaji kama nakosea
Shahidi: Sina kumbukumbu
LISSU VS SHAHIDI KUHUSU KATIBA MPYA
Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu kama haya madai ya katiba mpya na mfumo uhuru wa uchaguzi ni madai ambayo yamekuwepo kwa zaidi ya miaka 35 katika nchi hii
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama unafahamu kuwa mwaka 1992 Tume ya Nyalali ilipendekeza itungwe katiba mpya itakapofikia Septemba 2003
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu au hufahamu mapendekezo haya yalikataliwa na CCM
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama unakumbuka mwaka 1998 Rais Mkapa aliunda tume ya Jaji Kisanga ikapendekeza kuwe na katiba mpya halafu Mkapa akasema hadharani sikuwatuma waangalie masuala ya Katiba mpya
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama unafahmu au hufahamu mwaka 2003 Mkapa aliunda tume iliyoongozwa na Jaji Mark Bomani na tume ikapendekeza kuwe na katiba mpya kwa ajili ya nchi yetu na serikali ya Mkapa na CCM ikakataa
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama unafahamu au hufahamu kwamba mwaka 2011 Rais Jakaya Kikwete aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba maarufu kama Tume ya Warioba na sio tu ilipendekeza Katiba mpya ilitegeneza Rasimu ya Katiba Mpya
Shahidi:
Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kumekuwa na uchaguzi kila baada ya miaka mitano
Shahidi: Nafahamu
Lissu: Kila uchaguzi Mkuu watazamaji wa kimataifa wamependekeza ipatikane katiba mpya
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Uchaguzi Mkuu wa 2015 ilani ya CCM ilikuwa na ahadi watakamilisha mchakato wa katiba mpya baada ya uchaguzi mkuu
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Baada ya uchaguzi Rais Magufuli akasema suala la katiba hakuna
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze Majaji baada ya kutoa hotuba yangu April 3, 2025 kama wewe na Jeshi la Polisi mlichukua hatua yoyote ya kunitafuta kuniuliza haya maneno kukinukisha kuuvuruga uchaguzi yana maana gami
Shahidi: Sio kweli
Lissu: Hamkutafuta ufafanuzi wa hayo maneno yangu…nitakuwa sahihi au si sahihi nikisema kwamba kwa miaka yote 35 no reform no election ilikuwa ni msimamo sahihi katika mazingira ya aina hii
Shahidi: Haukua sahihi
Lissu: (Akirejea ripoti ya Jaji Chande Ukurasa wa 11 juu ya katiba mpya akidai kuwa hata Tume ya Jaji Chande iliafiki msimamo wa CHADEMA ni sahihi)
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Februari 13 mwaka huu kikosi kazi cha Kamati ya Haki za Binadamu kimetoa taarifa baada ya miezi sita walipendekeza nilipwe fidia kwa uonevu niliofanyiwa.
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu Mwezi uliopita Julai 10 Kamati ya Mawaziri wanaowakilisha nchi za Jumuiya za Madola imetoa taarifa inayotaka serikali ya Tanzania kuniachia huru bila masharti yoyote ndani ya siku 30 na wakasema serikali isipofanya hivyo kwenye kikao cha Septemba mwaka huu serikali ya Tanzania itashughulikiwa
Shahidi: Sifahamu
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji huyu mtu anayepiganiwa na taasisi hizi ni mhaini ni mtu mbaya anayestahili kunyongwa
Shahidi: Sijasema hivo
ACP MAHAMBA ALIVYOFAFANUA LISSU KUCHAPISHA VIDEO JAMBO TV
Baada ya hapo Lissu akawa ametamatisha maswali yake ya dodoso ambayo alitumia takribani dakika 40 kisha shahidi akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga aliulizwa maswali ya kusawazisha.
Katuga: Uliulizwa kuhusu maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka yanayosemekana na kusemwa na mshtakiwa tutakinukisha, tutazuia uchaguzi ukaulizwa kama kuna neno serikali ukasema halipo fafanua
Shahidi: Waheshimiwa Majaji nilipotamka neno serikali lipo nilikuwa namaanisha kwamba serikali ndiyo yenye mamlaka wajibu wa kutekeleza na kusimamia sheria za nchi katika maneno kama hayo kwamba tutazuia uchaguzi au kuvuruga uchaguzi maana yake ni kuitishia serikali ambayo ndiyo yenye dhamana ya kulinda amani ya nchi.
Katuga: Naomba ufafanuzi kwenye majibu uliulizwa nani aliyechapisha mtandaoni maneno ya vitisho kwa serikali ukajibu ni wewe mshtakiwa ukapelekwa mbali kusomeshwa maelezo ya mashahidi waliotoa ushahid anaitwa P wanaeleza nini kwamba wao ndio Waliosambaza hiyo video P na P1 ukasomeshwa maelezo ya George Bagyemu ukasema Bwana Bagyemu aliona video kwenye ukurasa wa Jambo bado ukasema wewe ndiye ulichapisha tufafanulie
Shahidi: Nilikuwa namaanisha mshtakiwa ndiye alikuwa akiongea mbele ya waandishi wa habari ambao walikuwa wakirusha matangazo live kwamba hilo lilikuwa ni nia yake halafu kama alikuwa hataki yale matangazo yarushwe mubashara asingewaruhusu kwa sababu walikuwa mbele yake.
Katuga: Kwa hiyo ndiyo maana ukakomaa ni wewe
Shahidi: Ndio
Katuga: Ukasomeshwa kifungu cha 39(2)(d) cha kanuni ya adhabu sura ya 36 ya Penal Code ukaulizwa haya maneno kuzuia uchaguzi kukinukisha yapo kwenye kifungu ulisisitiza yapo
Shahidi: Nilikuwa namaanisha kwamba nia ya kutisha serikali kwa hiyo yale maneno ambayo yalitamka mshtakiwa tutazuia uchaguzi tutahamasisha uasi tafsiri yake alikuwa na hiyo nia ya kutisha serikali
Katuga: Umeulizwa sana kuhusiana na katiba kuhusianisha na kosa hili la uhaini ifafanulie mahakama hayo mambo ya madai ya katiba na leo hii kosa la uhaini ulimaanisha nini majibu yako kwenye hili
Shahidi: Hayahusiani
Katuga: Umeulizwa kama umeeleza sababu ya utofauti wa maelezo yako polisi na ushahidi ukajibu sijaeleza tufafanulie
Shahidi: Ni kweli sijaeleza lakini ninachofahamu yale niliyoandika nikiwa ofisini na maelezo niliyotoa nikiwa hapa mahakamani majibu niliyotoa yalikuwa yanatokana na maswali niliyoulizwa.
Baada ya hapo jamhuri ikawa imetamatisha maswali ya Re-examination na shauri liliahirishwa huku Majaji wakiutaka upande wa jamhuri kuhakikisha uwepo wa mashahidi wa kutosha kesho mahakamani.