Latest Posts

MFANYABIASHARA WA KARIAKOO AFIKISHWA MAHAKAMANI ILALA: ASHTAKIWA KWA KUMSHAMBULIA ASKARI POLISI NA KUTISHIA KUUA

Mfanyabiashara wa Kariakoo na mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam, Peter Mmasi (32), leo Jumatano, Novemba 18, 2026, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili ya kumshambulia askari polisi na kumzuia kutekeleza majukumu yake ya kisheria.

Kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa leo mahakamani hapo, ambapo mshtakiwa huyo anawakilishwa na mawakili wake.

Kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa huyo kunafuatia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam mnamo Novemba 11, 2026, iliyoeleza kuwa lilikuwa likimshikilia na kumhoji kwa kina Peter Mmasi kuhusiana na tukio la kumshambulia Sajenti Johnson Sylivery, ambaye wakati wa tukio alikuwa akitekeleza wajibu wake wa kisheria wa kumkamata mtuhumiwa huyo.

Jitihada za kukamatwa kwa Mmasi zilifuatia malalamiko na tuhuma za kutishia kumuua raia mmoja aliyetajwa kwa jina la Carisma Amedeus Kileo, ambaye pia ni mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!