Latest Posts

HUDUMA ZA POLISI KUSOGEZWA KARIBU NA WANANCHI KOROGWE

Wananchi wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga sasa kunufaika na huduma za kipolisi karibu na makazi yao kufuatia kujengwa kwa kituo cha polisi, baada ya awali kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Wakizungumza na waandishi wa habari Novemba 17, 2026, katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kituo hicho cha polisi lililowekwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camilius Wambura, wananchi hao wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo, wakisema sasa huduma za kipolisi zimewasogelea na hivyo kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kuzifuata.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camilius Wambura, wakati akiweka jiwe la msingi katika kituo hicho, amewataka wananchi wa eneo hilo kujiepusha na vitendo vya uhalifu vinavyoweza kuwaingiza kwenye matatizo ya kisheria na kusababisha kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Mradi huo unatekelezwa kwa mfumo wa nguvu kazi, huku gharama za utekelezaji wake zikifikia zaidi ya shilingi milioni 809.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!