Latest Posts

VIJANA 80 BBT UVUVI MWANZA KUVUNA FAIDA YA MILIONI 9 KILA MMOJA

Vijana 80 wanufaika wa programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) Uvuvi jijini Mwanza wanatarajia kujipatia kipato cha zaidi ya Milioni 9 kila mmoja ikiwa ni matunda yanayotokana na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kwa kipindi cha miezi saba.
Akizungumza leo kwenye uzinduzi wa uvunaji wa Samaki kwenye vizimba chini ya Programu ya BBT – Uvuvi Meneja wa Kituo cha Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Kampasi ya Nyegezi, Peter Masumbuko amesema uwekezaji wa kizimba kimoja unafikia milioni 25 huku gharama za uendeshaji zikiwa takribani milioni 17, hali inayomwezesha mnufaika kupata faida hiyo kila mmoja.
“Kizimba kimoja uwekezaji wake ni takriban milioni 25 sasa tukitoa zile gharama za uendeshaji, takriban milioni 17, faida anayopata kijana ni milioni 9 ukigawanya kwa kipindi hicho cha uzalishaji nill kijana ana uwezo wa kuingiza milioni moja kwa mwezi kiasi ambacho kwa kweli ni kikubwa ukilinganisha na mwajiliwa wa serikali,”
 Akizungumza mara baada ya kuzindua zoezi hilo  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka amesema mafanikio hayo yanatokana na mfumo wa uwezeshaji unaojumuisha mafunzo ya miezi mitatu, mikopo isiyo na riba wala dhamana pamoja na usimamizi wa karibu katika kipindi chote cha uzalishaji.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!