Latest Posts

USAWA WA KIJINSIA WAPEWA THAMANI KATIKA MINYORORO YA THAMANI YA KILIMO

 

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeendesha mafunzo ya siku tatu kwa watoa huduma za maendeleo ya biashara za kilimo (ABD Service Providers) na wadau wa masoko, yakilenga kuimarisha usawa wa kijinsia, haki za wanawake na ushiriki wa makundi yaliyo pembezoni katika minyororo ya thamani ya kilimo.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, yakilenga kuongeza uelewa wa wadau kuhusu nafasi ya wanawake na namna ya kuwawezesha kupata fursa sawa za kiuchumi katika sekta ya kilimo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba, amesema washiriki kutoka sekta binafsi, wauzaji wa pembejeo, taasisi za fedha, wafanyabiashara, serikali za mitaa na Asasi za Kiraia wamekusanywa ili kujenga uelewa na ushirikiano wa pamoja katika kuimarisha ushiriki wa wanawake kwenye minyororo ya thamani ya kilimo.

Temba amesema mafunzo hayo yanajadili pia masuala ya mabadiliko ya tabianchi, matumizi endelevu ya rasilimali asilia na uhifadhi wa mazingira, pamoja na nafasi ya wadau katika kujenga minyororo ya thamani ya kilimo yenye tija na ustahimilivu.

Mratibu wa Mradi kutoka TGNP, Mariam Oushoudada, amesema kupitia Mradi wa Ustahimilivu Wake, Dunia Yetu (HROP), wanaimarisha uwezo wa wanawake na vijana kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kushiriki katika shughuli za kiuchumi zinazotokana na rasilimali za mazingira.

Amesema mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Canada kwa miaka sita na kuratibiwa nchini na CARE International, kwa kushirikiana na Shahidi wa Maji, AGCOT Centre Limited (SCL), WWF na Conservation Farming Unit Tanzania, ukiwalenga zaidi wanawake na vijana wanaotegemea rasilimali za mazingira katika maeneo yanayozunguka Mto Mkuu wa Ruaha.

Mafunzo hayo yataendelea hadi Septemba 3, 2026, katika Ukumbi wa NFS mjini Mafinga, yakilenga kujenga minyororo ya thamani ya kilimo inayozingatia usawa wa kijinsia, ustahimilivu wa jamii na fursa sawa za kiuchumi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!