Latest Posts

MAKONDA AENDA BARCELONA KUTAFUTA USHIRIKIANO WA KUKUZA VIPAJI TANZANIA.

Na Jerry Gregory,

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameanza ziara maalum ya siku nne nchini Hispania kwa lengo la kujadili fursa za ushirikiano kati ya Tanzania na klabu ya FC Barcelona katika maendeleo ya soka.

Makonda yupo nchini humo kufuatia mwaliko wa Rais wa FC Barcelona, Joan Laporta, ambapo mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita katika namna klabu hiyo inaweza kushirikiana na Tanzania katika kukuza vipaji vya soka na kuboresha maendeleo ya mchezo huo nchini.

Katika ziara hiyo, maeneo yanayotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na ukuzaji wa vipaji, maendeleo ya kiufundi, uendeshaji wa timu za taifa pamoja na namna uzoefu wa Barcelona unavyoweza kutumika kusaidia maandalizi ya Tanzania kuelekea michuano ya AFCON 2027.

Ushirikiano huo unalenga pia kujenga fursa ambazo zinaweza kuwasaidia vijana wenye vipaji kupata mazingira bora ya kukuza uwezo wao, huku Tanzania ikinufaika na uzoefu wa moja ya klabu kubwa na zenye historia katika maendeleo ya soka duniani.

Kwa upande wake, Joan Laporta alitumia fursa ya kukutana na Makonda kutoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mumewe, Mzee Hafidh Ameir Hassan, kilichotokea Septemba 7, 2026.

Ziara hiyo ya Makonda inatarajiwa kufungua mjadala mpana kuhusu namna Tanzania inavyoweza kutumia uzoefu na mifumo ya klabu kubwa za kimataifa katika kujenga vipaji, kuimarisha ufundi na kuinua kiwango cha soka nchini.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!