Latest Posts

MATAIFA 48 KUTUA ARUSHA KWA MKUTANO WA CATA, WAGENI ZAIDI YA 100 KUTALII TANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla, amesema kuwa zaidi ya wajumbe 100 kutoka mataifa 48 wanatarajiwa kuwasili jijini Arusha kuhudhuria Mkutano wa 46 wa Wakuu wa Mamlaka za Kodi za Jumuiya ya Madola (CATA), utakaofanyika kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Septemba 30, 2026, jijini Arusha, CPA Makalla amesema mkutano huo utafunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, mnamo Oktoba 6 katika Hoteli ya Grand Melia.

Amebainisha kuwa kaulimbiu ya mkutano huo inalenga matumizi ya teknolojia katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato, jambo ambalo litatoa fursa kwa Tanzania kujifunza mbinu bora za kimataifa, kujenga uwezo kwa wataalamu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na kukabiliana na changamoto za biashara zinazovuka mipaka.

Sambamba na hilo, CPA Makalla amewataka wananchi na watoa huduma Arusha kutumia fursa hiyo kuwahudumia wageni kwa ukarimu na upendo, akisema wajumbe hao watatumia hoteli, usafiri na huduma mbalimbali wakati wa kukaa jijini humo.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Mcha Hassan Mcha, ameeleza kuwa mbali na teknolojia na uchumi wa kidijitali, mkutano huo utajadili masuala ya kuboresha huduma kwa walipakodi ili kufikia viwango vya kimataifa na kubadilishana uzoefu wa kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia katika mifumo ya kodi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!