Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Jukwaa la Mabunge la Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR), unaofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
Mkutano huo muhimu, pamoja na ajenda nyingine, ni kielelezo cha jitihada kubwa zinazofanywa kuwainua wanawake na nafasi yao muhimu katika kuimarisha uongozi, kudumisha amani na kuchochea maendeleo endelevu.

Pia, ni kudhihirisha dhamira ya kuendeleza misingi ya mshikamano, usawa na ushirikiano wa Kiafrika, ambayo imekuwa sehemu muhimu ya historia ya Bara la Afrika.
Historia ya jukwaa hilo inakumbusha nafasi ya kipekee ya Tanzania katika kuhimiza mshikamano na ushirikiano wa kikanda.
