Latest Posts

“KISINGIZIO CHA VITA SIO SAHIHI”, ACT YAIAMSHA CCM KUHUSU MAISHA MAGUMU NA HATARI YA WANANCHI KUKOSA MLO

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu ameitaka Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuumiza kichwa na kuchukua hatua za haraka za kuboresha maisha ya Watanzania wa hali ya chini, huku akikosoa mchakato wa ununuzi wa mafuta na kile alichokiita tozo nyingi zinazozidi kuwaumiza wananchi.

Semu ameyasema hayo jioni ya leo Novemba 3, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kasimbu, Uwanja wa Mwembe Mmoja mkoani Kigoma, ambapo amedai kuwa Serikali imemsahau Mtanzania wa kawaida ambaye kwa sasa anahaha na ugumu wa maisha na hatari ya kukosa hata mlo mmoja

“Upande wa mafuta ya nishati. Kisingizio cha vita sio kisingizio sahihi. Usahihi ni kwamba serikali imeachia ununuzi wa mafuta umekuwa ununuzi wa kiholela, ununuzi usiomzingatia mlaji wa mwisho, ununuzi unaokwenda kuwaneemesha watu wachache. Lakini serikali imeweka tozo kubwa inayoelemea bei ya mafuta, kuna tozo mbalimbali. Haya mafuta yanapotufikia tayari yameshaongezwa tozo mbalimbali zaidi ya tozo 19… Na mtu anayekwenda kubeba gharama ya hizi tozo ni mlaji wa mwisho ambaye ni mimi na wewe”, ameeleza.

Aidha, Semu ameihimiza Serikali kuingilia kati udhibiti wa bidhaa muhimu za ujenzi na chakula, akiitaka isimamie kikamilifu uingizaji wa sukari na simenti ili kuhakikisha bei za bidhaa hizo zinashuka na kumwezesha mwananchi wa hali ya chini kumudu maisha.

“Tunaitaka serikali tunaiamsha serikali ya Chama cha Mapinduzi kwamba imemsahau Mtanzania wa kawaida. Watanzania wanalia na maisha magumu. Sasa hivi hata mlo mmoja unakwenda kukosekana. Serikali imkumbuke mwananchi Mtanzania mtu wa hali ya chini. Serikali isimamie vibali vya sukari na sementi kutoka nje vizuiwe na ihakikishe bei ya sementi inashuka chini ili mtu wa kawaida aweze kumudu”, ameeleza Semu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!