Latest Posts

MAFUNZO YA LINDA USHIRIKA NAMTUMBO KUONGEZA TIJA NA UWAJIBIKAJI KWA WAKULIMA

 

Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dodoma, Consolata Kiluma, amewataka watendaji wa vyama vya ushirika wanaoshiriki mafunzo kupitia programu maalumu ya Linda Ushirika Chagua Uadilifu mkoani Ruvuma kuhakikisha wanatumia ujuzi wanaoupata kuboresha utendaji wa vyama vyao ili kuongeza tija kwa wakulima.

Wito huo umetolewa Novemba 6, 2026, wakati wa ziara yake wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, iliyolenga kukagua namna vyama vya ushirika vinavyojiendesha pamoja na kufuatilia changamoto zinazovikabili amesisitiza kuwa mafunzo hayo yanapaswa kuleta mabadiliko ya vitendo katika usimamizi wa vyama, uwazi na uwajibikaji ili kuhakikisha wakulima wanapata manufaa stahiki kupitia vyama vyao.

Kwa upande wake, Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Ruvuma, Venance Msafiri, amesema mafunzo hayo tayari yameanza kuonesha matokeo chanya mkoani humo. Ameeleza kuwa mpango uliopo ni kuhakikisha waandishi na mameneja wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) wanapatiwa vitendea kazi vya kisasa ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.

Naye Mratibu wa Mafunzo kutoka Chuo cha Ushirika Moshi, kwa kushirikiana na Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Songea na Namtumbo, Juma Mwanga, wameeleza matarajio yao kuwa mafunzo hayo yataimarisha usimamizi na mifumo ya kiutendaji, hatua itakayosaidia chama hicho kufikia lengo la kupata hati safi za ukaguzi kuanzia chama kikuu hadi vyama vya msingi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!