Latest Posts

WANANCHI WAGOMA KUZIKA, WAZUIA BARABARA KWA JENEZA; POLISI WAINGILIA KATI NA KUWAKAMATA 15

Hali ya hofu, taharuki, na sintofahamu imetawala miongoni mwa wananchi wa Kijiji cha Igongwe, kilichopo Kata ya Sitalike, Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, kufuatia kile walichokieleza kuwa ni kuzorota kwa usalama na kutokea kwa mauaji ya kikatili ya mkulima Seni Kibiriti (58) yanayohusishwa na mgogoro wa muda mrefu wa kugombea mbuga za kilimo cha mpunga. Tukio hilo limetokea kufuatia migawanyiko ya makundi mawili ya wananchi wanaogombania umiliki wa eneo hilo kupitia vyombo vya sheria.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Igongwe, Bw. Mayala Nkuba Mandilindi, ameeleza kuwa hali ya usalama ni tete mno kwani yeye mwenyewe amelazimika kukimbilia porini kujificha baada ya kutishiwa maisha na kikundi cha wakulima wapatao 90 wanaopinga uamuzi wa mahakama uliorejesha umiliki wa eneo hilo kwa umma, licha ya maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, ya kuwataka wananchi waendelee na kilimo huku ulinzi ukiimarishwa.

Kufuatia kifo cha Seni Kibiriti aliyevamiwa na kuuawa shambani kwake, wananchi walioghadhabishwa walichukua uamuzi wa kugoma kumzika na badala yake kuuchukua mwili wake ukiwa kwenye jeneza na kuuacha katikati ya barabara kuu, hatua iliyosababisha usafiri kusimama.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi lilichukua hatua za haraka za kutuliza ghasia hizo na kufanikiwa kuondoa vizuizi, ikiwemo jeneza hilo, katika eneo la Kijiji cha Sitalike. Katika operesheni hiyo iliyofanyika Novemba 6, 2026, Jeshi la Polisi limewakamata watu 15 wanaodaiwa kuhusika na kitendo cha kufunga barabara hiyo kuu ya Mpanda Sumbawanga, huku msako mkali ukiendelea kuwasaka wahusika wote walioshiriki katika mauaji ya marehemu Seni Kibiriti ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!