Madereva wa bodaboda 50 jijini Tanga wamenufaika na mafunzo ya udereva pamoja na kupatiwa leseni chini ya udhamini wa Tanga Yetu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwaongezea ujuzi na kuimarisha usalama barabarani.
Wakizungumza na waandishi wa habari Novemba 20, 2026, wakati wa kukabidhiwa leseni hizo, madereva hao wa bodaboda wameeleza changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo wanapokuwa barabarani bila kuwa na leseni za udereva.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodaboda jijini Tanga Mohamedi Chande amesema jambo hilo ni endelevu katika kuakikisha wanabunguza ajali za barabarani.
Chande ameendelea kuzitaka taasisi mbalimbali kujitokeza na kushirikiana katika kuwawezesha madereva wa bodaboda kupata leseni, huku akiwahimiza madereva hao kujitokeza kwa wingi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo.