Latest Posts

ALIYEANDIKA FACEBOOK KUWA ATAKUFA 2025, ANYWA SUMU BAADA KUAMBIWA MTOTO SI WAKE

Mwili wa Justine Mbaga (28), kijana aliyefariki dunia Februari 11, 2025, kwa madai ya kunywa sumu baada ya kupewa taarifa kuwa mtoto aliyekuwa akimhudumia si wake, umezikwa siku ya Jumatano Februrari 12, 2025 katika makaburi ya Magegele, Halmashauri ya Mji Makambako mkoani Njombe.

Taarifa zinaeleza kuwa Februari 9, 2025, familia ya binti aliyekuwa naye katika uhusiano ilimwita Justine Mbaga na familia yake, na kumweleza kuwa mtoto aliyekuwa akilea si wake, jambo ambalo linadaiwa kumsababisha kuathirika kisaikolojia na kuchukua uamuzi huo wa kujitoa uhai.

Baadhi ya majirani wa Justine Mbaga wamesema kifo chake kimewaacha na majonzi mazito, wakimtaja kuwa kijana mwenye maadili mema.

Kwa upande wake, Ratifa Kibiki, mama mzazi wa binti mwenye mtoto huyo, amesema waliamua kumuita Justine Mbaga na familia yake ili kuwaeleza ukweli kuwa mtoto huyo si wake. “Tuliona si busara Justine aendelee kulea mtoto ambaye si wake, lakini binti yangu alikuwa tayari kumrejeshea gharama za matunzo alizotumia, ambazo ni shilingi 850,000.”

Diwani wa Kata ya Kitisi, Nevy Sanga, na Mtendaji wa Mtaa wa Kisingire wameiasa jamii kutochukua sheria mkononi na badala yake kutumia njia sahihi kushughulikia changamoto za kifamilia na mahusiano.

Taarifa za kifo cha Justine Mbaga zimezua mjadala mkubwa baada ya kuenea kwa habari kuwa kijana huyo alichapisha utambulisho kwenye ukurasa wake wa Facebook kabla ya kifo chake, akionesha kuwa alizaliwa mwaka 1997 na kufariki 2025, huku akihusisha kifo chake na masuala ya kifamilia na uhusiano.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!