Latest Posts

ARUSHA WAOMBWA KUSIMAMA NA MAMA OKTOBA 2025

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Namelok Sokoine, amewataka viongozi na wanachama wa CCM mkoani Arusha kuwa mstari wa mbele kujibu kwa hoja maudhui ya kejeli dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Namelok amesema hayo Juni 14, 2025, jijini Arusha, wakati wa mapokezi ya kumkaribisha nyumbani kwa cheo kipya, baada ya kuteuliwa Mei 28, 2025 na Rais Samia kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

“Halafu nawauliza, hivi hamuoni jinsi Rais wetu anavyotukanwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya watu? Nataka Mkoa wa Arusha uwe wa kwanza kukemea. Anzeni sasa kuwaambia watu mambo makubwa na mazuri anayoyafanya mama yetu.”

Pia, Namelok amewataka wajumbe wa kamati za maamuzi kutumia uwezo wao kikamilifu katika kuchuja wagombea wa nafasi mbalimbali watakaokata rufaa katika uchaguzi ujao.

Aidha amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Samia Suluhu Hassan kwa heshima kubwa kwa wana Arusha na Monduli. Ameahidi kulinda heshima hii kubwa aliyopewa na mwenyekiti kwa niaba ya Arusha na amewaomba Oktoba kusimama na Rais Samia kwa kumchagua kuwa Rais wa Tanzania.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!