Latest Posts

AWESO AFANYA MAZUNGUMZO NA BENKI YA EXIM YA KOREA, ANADI MIRADI YA MAJI

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametembelea na kufanya mazungumzo na Benki ya EXIM ya Korea ambayo ilitoa fedha za utekelezaji wa miradi ya majitaka nchini Tanzania yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 248.3 (takriban Shilingi bilioni 621.25). Miradi hiyo inalenga miji ya Dar es Salaam (Dola milioni 90, sawa na Shilingi bilioni 225.38), Dodoma (Dola milioni 70, sawa na Shilingi bilioni 175.51), na Iringa (Dola milioni 88.3, sawa na Shilingi bilioni 220.36).

Aidha, Makamu wa Rais wa Benki hiyo amesema kupitia EDCF na mifuko mingine Serikali ya Korea itaendelea kuisapoti Serikali ya Tanzania kupitia sekta ya maji katika uwekezaji zaidi wa utekelezaji wa miradi ya maji. Utekelezaji wa miradi hiyo utaimarisha huduma za usafi wa mazingira, kuondoa na kutibu majitaka.

Aidha, Tanzania imenufaika na msaada wa Dola za Kimarekani milioni 8 (takriban Shilingi bilioni 20.05) kutoka Korea Environmental Industry and Technology Institute (KEITI) kwa ajili ya kujenga mfumo wa kisasa wa kusimamia huduma za maji (Smart Water Management System) katika Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA). Mfumo huu utaifanya IRUWASA kuwa mamlaka ya kwanza nchini kutumia teknolojia hiyo, ambayo inalenga kudhibiti upotevu wa maji, kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuboresha huduma za maji kwa ufanisi zaidi.

Katika ziara hiyo, Aweso alikutana na wadau wa sekta ya maji kutoka taasisi za Korea, zikiwemo K-Water na kampuni zingine, hatua iliyosaidia kufungua milango ya ushirikiano mpya katika maeneo ya mafunzo kwa watumishi wa sekta ya maji, kubuni miradi mipya, na kutafuta fedha za utekelezaji wa miradi hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!