Latest Posts

MAHUNDI: WAZAZI MSIWAACHE WATOTO PEKE YAO

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi, amesema wazazi na walezi wana wajibu wa kuwa karibu na watoto wao, kuwafuatilia, kuwasikiliza na kuwapatia mwongozo unaofaa ili kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika maisha.
‎
‎
‎Mhandisi Mahundi ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa Mahafali ya 12 ya Darasa la Saba na Mahafali ya 8 ya Kidato cha Nne katika Shule ya St. Monica Moshono nakuongeza kuwa malezi ya mtoto hayapaswi kuangalia mafanikio ya kitaaluma pekee, bali yanapaswa kuzingatia makuzi na ukuaji wa kimwili, kiroho, kitabia na kitaaluma, huku akisisitiza kuwa mafanikio ya mtoto yanahitaji ushirikiano wa familia, shule, jamii na Serikali.


‎
‎Amesema wazazi na walezi wana wajibu wa kuwa karibu na watoto wao, kuwafuatilia, kuwasikiliza na kuwapatia mwongozo unaofaa ili kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika maisha.
‎
‎Aidha, amesema mabadiliko ya teknolojia yameleta fursa mbalimbali kwa watoto katika kujifunza na kupata taarifa, lakini pia yameibua changamoto zinazohitaji uangalizi wa karibu kutoka kwa wazazi, walezi na walimu
‎
‎Awali, akisoma taarifa ya shule hiyo, Mkuu wa shule hiyo Yuster Andrea Mbilinyi amesema shule imeendelea kuweka mkazo katika elimu, malezi na makuzi ya wanafunzi ili kuwajenga kuwa watu wenye nidhamu, maadili na uwajibikaji katika jamii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!