Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemteua tena Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman (OMO) kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 18, 2026 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mansura Kassim, uteuzi huo umeanza rasmi leo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais mteule ataapishwa Jumanne, Septemba 22, 2026, saa 4:00 asubuhi katika hafla itakayofanyika Ikulu, Zanzibar.
Othman Masoud Othman aliwahi kushika nafasi hiyo kuanzia Machi 2021, baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuchukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, aliyefariki Februari 2021.