Na. Fredrizzo Samson.
Katika kuadhimisha kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick North Mara imepeleka tabasamu kwa wananchi wanaoishi karibu na mgodi huo kwa kuwapatia majiko ya mitungi ya gesi.
Mgodi huo kupitia maneja wake, Apolinary Lyambiko umekabidhi majiko ya mitungi ya gesi 220 kwa wanawake wa vijiji vinavyouzunguka mgodi huo, ambao awali ilitanguliwa na elimu ya utumiaji.
Pia, mgodi huo, umetoa hundi ya billion 2.1 (Mrabaha ambao mgodi hutoa kwa kila robo ya mwaka na hii ni robo ya tatu kwa mwaka huu 2024) Nyabigena katika vijiji 5 vinavyouzunguka mgodi huo, ikiwa ni sehemu ya ushirikiano baina yake na wananchi wa mkoa wa Mara hususani katika vijijini 11 vinavyouzunguka mgodi huo uliopo Nyamongo Tarime Vijijini.
Akikabidhi hundi hizo kwa wenyeviti wa vijiji kwa niaba ya mgodi Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima ambaye amekuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo katika viwanja vya shule ya Ingwe Sekondari ameutaja mgodi huo kuwa chachu ya maendeleo ya mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla.
Sambamba na michango mbalimbali ya kimaendeleo inayofanywa na mgodi huo ikiwemo miundombinu ya barabara, shule, huduma za maji na kuwezesha vikundi mbalimbali vya kijasiriamali ikiwemo shamba darasa.
Akizungumza na Jambo TV kwa niaba ya wenyeviti wenzake wa vijiji, Zacharia Machage ambaye ni mwenyekiti wa Kijiji cha Nyangoto amesema mgodi huo umekuwa na mahusiano mazuri na wananchi wa vijiji vinavyouzunguka mgodi huo.
“Mgodi umekuwa na mahusiano mazuri na wananchi hasa kwa kushirikiana katika nyanja za kimchezo na kimaendeleo pia umekuwa ukitizima wajibu wa takwa la kisheria kama Serikali yetu ivyoelekeza tunaishukuru sana,” amesema Zacharia.
Habari hii kwa njia ya video Tembelea YouTube channel yetu #Jambo TV