Latest Posts

CHADEMA NYASA: TUHAKIKISHE KILA KITUO MAJINA YAMEBANDIKWA KWA USAHIHI

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Nyasa umewataka viongozi wake katika maeneo mbalimbali pamoja na wananchi kuhakikisha wanaweka mapingamizi wanapobaini kasoro mbalimbali baada ya zoezi la uandikishaji wapiga kukamilika mwishoni mwa juma lililopita.

Hayo yameelezwa na Katibu wa CHADEMA kanda ya Nyasa Grace Richard Shio wakati akizungumza na wanahabari juu ya mchakato unaofuata wa uchukuaji na urejeshaji fomu za kuomba kugombea nafasi mbalimbali za kiserikali ndani ya chama hicho.

Bi. Grace Shio anasema zoezi hilo litaanza Oktoba 26 hadi Novemba mosi, 2024 ambapo amewapongeza kwa kujiandikisha ili kuchagua viongozi wanaowataka.

Kiongozi huyo mtendaji wa CHADEMA Nyasa amesema Chama kimeweka nguvu katika kuhimiza kuhakikisha tarehe 26 Oktoba wagombea wote wa CHADEMA watachukua fomu na kuzirejesha Oktoba 30, 2024.

“Sisi kanda ya Nyasa kwa umuhimu na upekee wa uchaguzi huu tumeweka nguvu na tunawataka na kuwaomba wanachama wetu na wagombea wetu wote kuhakikisha tunachukua fomu kwa pamoja tarehe 26, Oktoba kila mmoja na tutapata utulivu wa kuzijaza fomu hizo na kuzirejesha Oktoba 30, 2024. Kwahiyo tuzingatie hizo tarehe kwa kanda yetu ya Nyasa na tunazo sababu maalum”, ameeleza Shio na kuongeza;

“Na suala lingine kuanzia sasa hivi tufuatilie kwenye vituo vya uandikishaji tuhakikishe kila kituo majina yamebandikwa kwa usahihi, tupitie hayo majina na tuweke mapingamizi pale tunapoona inafaa kwa mfano unakuta mtu sio mkazi wa eneo hilo tafadhali weka pingamizi, unawezakuta vijana wadogo chini ya umri wa miaka 18 wameandikishwa tafadhali weka pingamizi lakini pia kuna watu sio raia wa Tanzania na wamejiandikisha weka pingamizi na zoezi la mapingamizi litaenda mpaka tarehe 28, 2024”, amesisitiza Katibu wa CHADEMA kanda ya Nyasa Grace Shio.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!